Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na baadhi ya viongozi wa jeshi tayari wamewasili mjini humo Jumamosi kabla ya ziara hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa ziara hiyo ilikuwa inasubiriwa kufuatia mlipuko wa volcano wa Mlima Nyiragongo wiki mbili zilizopita.
Rais Tshisekedi anatembelea mashariki mwa nchi wakati ambapo kuna hali ya dharura iliyowekwa karibu wiki moja iliyopita katika juhudi za kupambana na makundi ya waasi.
Shirika la madaktari wasio na mipaka, MSF, linaasema ukiukwaji wa haki za binaadamu unaofanywa na waasi umekithiri katika mikoa ya kivu kaskazini na Ituri.
Vyanzo vya habari vinaeleza kuwa wapiganaji wanaodhaniwa kuwa ni wa kikundi cha waasi wa ADF waenedelea kushambulia na kuwaua wananchi.