Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 19:57

Serikali ya DRC yasema hakuna mlipuko wa pili wa volcano

Wakazi wa Goma wakusanyika kwenye kituo cha maji wakati ikiwepo hofu ya mlipuko mpya wa volcano karibu na kulikotokea mlipuko mwengine wiki moja iliyopita kwenye mlima Nyiragongo, Ijumaa, Mei 25, 2021.(Photo by Moses Sawasawa / AFP).

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imetangaza Jumamos kuwa habari zilizotolewa awali na serikali hiyo ya Kinshasa kuwa kulikuwepo na mlipuko mpya wa volcano karibu na kulikotokea mlipuko mwengine wiki moja iliyopita kwenye mlima Nyiragongo si za kweli. 

Wizara ya habari na mawasiliano kwenye ujumbe wa Twitter inaeleza kwamba lilikuwa onyo lisilo sahihi kuhusiana na mlipuko kwenye mlima Nyamulagira.

Wizara imeeleza kwamba picha zilizochukuliwa kwa ndege iliyo safiri kwenye eneo hilo la volcano zinaonyesha hakuna mlipuko wowote wa volcano na hakuna kitisho chechote kwa makazi ya maeneo ya kaskazini mwa mlima huo Jirani na ule wa Nyiragongo.

Taarifa ya wizara ya habari imeendelea kueleza kwamba moshi ulionekana na kusababisha kutolewa onyo ulitokana na kuchomwa kuni kwa ajili ya kupata mkaa, pamoja na wakulima kuchoma nyasi na kusababisha moshi mkubwa.

Mapema Jumamosi msemaji wa serikali alikuwa ametaja mlipuko kwenye mdomo wa volcano wa Murara kando ya volcano ya mlima Nyamuragira unaofahamika kua ni volcano yenye kutokota.

Watu wapatao 400,000 wameukimbia mji wa Goma mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo kufuatia onyo la kuripuka tena kwa volkano katika Mlima Nyiragongo.

Wananchi waliokimbia mlipuko wa volcano Goma, Congo, wakikusanyika katika kituo cha kugawa chakula Ijumaa, Mei 28, 2021 huko Sake, takriban kilomita 25 (maili 16) Magharibi ya Goma walipopata hifadhi. (AP Photo…

Maafisa wa Goma wamesema familia 80,000 ambazo ni sawa na watu 400,000 waliondoka Goma Alhamisi kufuatia tahadhari iliyotolewa na serikali.

Wakati huohuo vyanzo vya habari vinaeleza serikali ya Congo inafanya jitihada za kutoa misaada ya maji ya kunywa, chakula na vifaa vingine na wafanyakazi wanasaidia kuwakutanisha watoto waliotengana na familia zao.

Awali, ofisi ya Umoja wa Mataifa inayoratibu misaada ya kiutu, OCHA, ilikadiria kuwa takriban watu 400,000 kati ya 600,000 wa mji huo wataathirika na agizo hilo ambalo limetolewa kwenye wilaya 10 kati ya 18.

Hadi sasa taarifa zinaeleza kuwa watu 34 wamekufa kutokana na athari za mripuko huo wa volkano wa juma lililopita.

XS
SM
MD
LG