Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 05:31

Algeria kufanya uchaguzi wa bunge Jumamosi


Waandamanaji kwenye mji mkuu wa Algeria wa Algiers katika picha ya awali.
Waandamanaji kwenye mji mkuu wa Algeria wa Algiers katika picha ya awali.

Algeria inafanya uchaguzi wa bunge Jumamosi wakati vuguvugu la maandamano likisihi wapiga kura kususia huku kukiwa na wasi wasi kwamba taifa hilo la Afrika kaskazini linaweza kujikwamua kutoka kwenye janga la kisiasa na kiuchumi.

Zoezi hilo linafanyika wakati serikali ikijaribu kuimarisha uhalali wake huku ikikabiliana na vuguvugu la Hirak, ambalo limerejea tena barabarani mwezi Februari baada ya kusitisha maandamano kwa karibu mwaka mmoja kufuatia janga la corona.

Mwaka wa 2019, Hirak liliongoza maandamano ya maelfu ya watu na kupelekea kujizulu kwa kiongozi wa muda mrefu wa taifa hilo Abdelaziz Bouteflika baada yake kutangaza nia ya kuwania urais kwa muhula wa tano.

Uchaguzi wa urais uliyofanyika miezi 18 iliyopita ulishindwa na Abdelmadjid Tebboune wakati ukiwa na chini ya asilimia 40 ya wapiga kura walioshiriki kulingana na takwimu rasmi.

Alhamis kiongozi wa upinzani Karim Tabbou alikamatwa karibu na nyumba yake kulingana na ripoti iliyotolewa na ndugu yake. Habari kutoka vyombo vya habari vya ndani zinasema kuwa mkurugenzi wa Radio M, Ishane El Kadi pia amezuiliwa.

Imetayarishwa na Harrison Kamau

XS
SM
MD
LG