Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 16:51

Naftali Bennett ameapishwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Israel


Naftali Bennett, Waziri Mkuu mpya wa Israel
Naftali Bennett, Waziri Mkuu mpya wa Israel

Bennett atakuwa Waziri Mkuu kwa miaka miwili kwa mujibu wa makubaliano yasiyo ya kawaida ya kushirikiana madaraka miongoni mwa vyama vinane vya kisiasa vyenye mtizamo mdogo wa  pamoja isipokuwa kutaka kumaliza uongozi wenye mzozo wa Netanyahu

Serikali mpya ya Israel iliapishwa Jumapili na kumaliza utawala wa miaka 12 wa Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu na kumfanya Naftali Bennett, mkuu wa chama kidogo cha kidini kuwa kiongozi mpya wa taifa la wayahudi.

Bennett atakuwa Waziri Mkuu kwa miaka miwili kwa mujibu wa makubaliano yasiyo ya kawaida ya kushirikiana madaraka miongoni mwa vyama vinane vya kisiasa vyenye mtizamo mdogo wa pamoja isipokuwa kutaka kumaliza uongozi wenye mzozo wa Netanyahu.

Waziri Mkuu mpya wa Israel, Naftali Bennett
Waziri Mkuu mpya wa Israel, Naftali Bennett

Naftali Bennett ni mshirika wa zamani wa Netanyahu ambaye alihudumu kama waziri wake wa ulinzi mwaka 2019 na mwaka 2020. Bennett mwenye umri wa miaka 49 baada ya miaka miwili atamuachia uongozi Yair Lapid, mwenye miaka 57 ambaye aliwahi kuwa waziri wa fedha na mtangazaji wa zamani wa habari kwenye TV ndiye alisimamia mpango huo wa kumuondoa Netanyahu.

Lapid alishinda kura ya pili kwa kishindo akiwa nyuma ya chama cha Netanyahu cha LIKUD hapo mwezi Machi, uchaguzi wa nne usiotoa maamuzi kwa Israel katika kipindi cha miaka miwili iliyopita.

XS
SM
MD
LG