Shirika hilo liitwalo Kiswahili Network Canada, lina wanachama 150, wengi wao wanapatikana mikoa ya Quebec na Montreal. Moja kati ya malengo yake, ni kuwafunza Kiswahili watoto walioazaliwa Canada, kama anavyosema naibu mwenyekiti wa shirika hilo, Juma Manirambona kutoka Burundi.