Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 15, 2025 Local time: 08:30

Canada yaongeza idadi ya wahamiaji kukabiliana na upungufu wa nguvu kazi


Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau
Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau

Canada imeweka rekodi ya uhamiaji mwaka 2022 kwa kutoa vibali vya ukaazi wa kudumu kwa zaidi ya wageni 437,000, serikali ilisema Jumanne, ikiongeza idadi ya wahamiaji kukabiliana na upungufu wa nguvu kazi katika soko la ajira.

Serikali ilikuwa imeweka lengo la kukaribisha wakazi wapya wa kudumu 431,645 mwaka 2022, na wizara ya uhamiaji ilisema Canada ilifikia lengo kwa kupokea idadi ya juu kabisa ya watu katika historia ya Canada.

Majumuisho ya mwaka jana ni 9% ikiwa ni juu kuliko rekodi mwaka 2021, wakati Canada ilipovuka rekodi yake ya awali iliyowekwa 1913, na imekuja wakati Canada inataka kuingiza wakazi wapya wa kudumu milioni 1.45 ifikapo mwaka 2025.

Uhamiaji ni sehemu muhimu ya suluhisho wakati Canada ikilenga katika kutatua uhaba mkubwa wa soko la nguvu kazi, wizara hiyo imesema. Watu wenye vibali vya ukaazi wa kudumu wanaweza kuomba uraia baada ya miaka mitano.

Uhamiaji unajumuisha takriban asilimia 100 ya ukuaji wa nguvu kazi ya Canada na ifikapo 2036 wahamiaji watakuwa kiasi cha 30% ya idadi ya watu Canada, ikiwa ni ongezeko kutoka 20.7% mwaka 2011, taarifa hiyo imesema.

Kituo cha Kiislam Quebec Islamic Cultural Center, Canada
Kituo cha Kiislam Quebec Islamic Cultural Center, Canada

Serikali ya Waziri Mkuu Justin Trudeau imekuwa ikitegemea wahamiaji kuboresha uchumi wa Canada na kusaidia kukabiliana na ongezeko la idadi kubwa ya wazee tangu alipoingia madarakani mwaka 2015.

Uhaba wa wafanyakazi wenye ujuzi katika sekta kama vile huduma za afya ni mkubwa na takwimu rasmi za hivi karibuni kabisa zinaonyesha kulikuwa na nafasi za kazi 871,300 mwezi Oktoba, ikiwa idadi ya chini kutoka rekodi ya juu ya zaidi ya nafasi milioni moja zilizokuwa wazinchini Canada mwezi Mei.

XS
SM
MD
LG