Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 10:49

Papa Francis aelekea Canada kwa "ziara ya kuomba msamaha"


Papa Francis muda mfupi kabla ya kuondoka mjini Roma kwa ziara nchini Canada Jumapili Julai 24, 2022
Papa Francis muda mfupi kabla ya kuondoka mjini Roma kwa ziara nchini Canada Jumapili Julai 24, 2022

Kiongozi mkuu wa kanisa Katoliki, Papa Francis, aliondoka mjini Roma mapema Jumapili kuelekea nchini Canada kwa ziara ambayo inatajwa kama ya kuomba msamaha wa moja kwa moja kwa waathiriwa wa unyanyasaji uliofanyika kwa muda wa miongo kadhaa katika shule za malazi zinazoendeshwa na Kanisa Katoliki.

Papa, anayeongoza kanisa lenye waumini wapatao bilioni 1.3 kote duniani alitarajiwa kulakiwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Edmonton na Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau.

Ndege iliyombeba iliondoka mjini Roma muda mfupi baada ya saa tatu asubuhi kwa saa za Italia.

Safari hiyo ya saa 10 ndiyo ndefu zaidi tangu 2019 kwa kiongozi huyo mkongwe, mwenye umri wa miaka 85, ambaye amekuwa akisumbuliwa na maumivu ya goti ambayo yamemlazimu kutumia kijiti au kiti cha magurudumu katika matembezi yake ya hivi karibuni.

Papa alikuwa kwenye kiti cha magurudumu siku ya Jumapili na alitumia jukwaa la kunyanyua kupanda ndege hiyo, mwandishi wa AFP aliyeandamana naye alisema.

XS
SM
MD
LG