Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 04:01

Canada kuwawekea vikwazo raia wa Iran


Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau.
Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau.

Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau alitangaza Jumatatu kwamba serikali yake itawawekea vikwazo "dazeni" ya watu na mashirika ya Iran, ikiwa ni pamoja na maafisa wa polisi wanaowaitwa "wa maadili," wakati vikosi vya usalama nchini Iran vikiendelea kukabiliana na waandamanaji.

Akihutubia "wanawake wanaoandamana nchini Iran na wale wanaowaunga mkono," Trudeau alisema: "Tuko pamoja nanyi."

Trudeau alisema Wakanada, pamoja na mamilioni ya watu duniani kote, wanataka serikali ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran "isikilize watu wake, kukomesha ukandamizaji wa uhuru na haki zao, na kuruhusu wanawake na watu wote wa Iran kuendelea na maisha yao bila kuingiliwa, na kutoa maoni kwa amani na utulivu."

"Tumewawekea vikwazo baadhi ya wanachama wa IRGC, na tutaendelea kuzingatia hatua nyingine zozote tunazoweza kuchukua kuhusiana na vikwazo hivyo," alisema.

Mnamo Januari 2020, Ndege ya Shirika la Ndege la Ukraine PS752 ilidunguliwa na makombora ya IRGC dakika chache baada ya kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Tehran, na kuua watu 176, wakiwemo darzeni ya raia wa Kanada.

Tangu wakati huo, serikali ya Canada imekuwa ikishinikizwa na makundi kadhaa, wakiwemo wahafidhina wa upinzani, kuchukua msimamo mkali zaidi dhidi ya Iran.

Maandamano yanayoendelea, ambayo yamekuwa yakitokea katika majimbo yote ya Iran, yalianza baada ya mwanamke Mahsa Amini kufariki akiwa mikononi mwa polisi.

XS
SM
MD
LG