Polisi nchini Canada, katika mji wa Ottawa, wanatarajia kuwaondoa barabarani madereva wa magari ya kubeba mizigo ambao wamekuwa katika mgomo kwa muda wa wiki tatu wakilalamikia amri za kuwataka kupata chanjo dhidi ya virusi vya Corona.
Maandamano hayo yameathiri shughuli katika mji huo na kumlazimu Waziri mkuu Justin Trudeau kutumia mamlaka yake ya dharura, kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 50.
Madereva hao wameungana na maelfu ya waandamanaji, huku magari karibu 400 yakiwa yameegeshwa barabarani tangu Januari 28.
Baadhi ya waandamanaji wamekamatwa akiwemo Chris Barber ambaye ni mmoja wa waandaaji wa maandamano hayo.