Jacobellis mwenye umri wa miaka 36 amekuwa aking’aa kwenye mchezo huo tangu ulipoanzishwa miaka michache iliyopita.
Sasa hivi anaonekana kufikia ndoto yake tangu kujiunga kwenye mchezo huo kwa mara ya kwanza mwaka wa 2006 wakati wa michezo ya Olimpiki ya msimu wa baridi mjini Turin, Italia.
Wakati huo nusra angepata dhahabu, lakini kwa bahati mbaya aliteleza na kuanguka wakati akiwa karibu kumaliza.
Chloe Tres-peuch wa Ufaransa naye alijipatia medali ya fedha, huku Meryeta Odine wa Canada akipata ile ya shaba.
Kufikia sasa Ujerumani inaongoza kwa kushinda kwenye michezo minne kwenye mashindano hayo yanayofanyika kwenye theluji. Miongoni mwa mataifa mengine yaliofanya vizuri kufikia sasa ni pamoja na Norway na Korea Kusini.