Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 11:31

Zelenskyy amewafuta kazi wakuu wa usalama, Russia imeongeza mashambulizi


Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy wakati aliwatembelea wanajeshi wa Ukraine katika eneo la Dnipropetrovsk July 8 2022. Picha: Reuters
Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy wakati aliwatembelea wanajeshi wa Ukraine katika eneo la Dnipropetrovsk July 8 2022. Picha: Reuters

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelenskyy amewafuta kazi mwendesha mkuu wa mashtaka na mkuu wa idhara ya usalama, ikiwa ni mabadiliko makubwa kuwahi kutekelezwa katika serikali yake tangu Russia ilipovamia nchi hiyo miezi mitano iliyopita.

Zelensky ametekeleza mabadiliko hayo huku wanajeshi wa Russia wakiwa wanaongeza mashambulizi kwa lengo la kutwaa sehemu kadhaa mashariki mwa Ukraine

Amesema kwamba hatua ya kumfuta kazi Mwendeshamkuu wa mashtaka Iryna Venediktova na mkuu wa usalama Ivan Bakanov inatokana na kuongezeka kwa kesi za uhaini dhidi ya maafisa wa usalama wa Ukraine.

"Kufikia leo, kesi za uhalifu 651 zimesajiliwa. Zinahusu uhaini na vitendo vingine vinavyowashirikisha wafanyakazi katika ofisi ya mwendesha mkuu wa mashtaka, idhara za upepelezi na idhara za usalama. Wahusika wamepewa taarifa kuhusu kesi za uhalifu 198. Zaidi ya wafanyakazi 60 katika ofisi ya mwendesha mkuu wa mashtaka na idhara ya usalama wamesalia ofisini na kuendelea kufanya kazi dhidi ya nchi yetu.”

Zelenzky vile vile amesema kwamba amemwambia waziri mkuu wa Canada Justin Trudeau katika mazungumzo yao kwa njia ya simu kwamba Ukraine haitawahi kukubali hatua ya Canada kuipatia Ujerumani bomba la kusafirisha mafuta la Nord stream, akisema kwamba Ujerumani inaweza kutoa bomba hilo kwa Russia, baadaye.

"Hili swala halihusu tu bomba la gesi. Hili ni swala la kuheshimu vikwazo. Haka ukiukwaji utafanyika sasa hivi kwa hili swala moja, ukiukwaji utafanyika kwa maswala mengine. Russia inafanya hivi kwa njia za kiujanja kuhusu gesi na kuchochea ukiukwaji wa vikwazo. Kuna njia za kutosha kwa gesi kutoka Russia kuingia ulaya na ni lazima kila nchi iheshimu kanuni zake.” Amesema rais Zelensky.

Zelensky vile vile amejibu matamshi ya onyo kutoka kwa naibu wa baraza kuu la usalama kwamba shambulizi lolote kuhusu dhidi ya daraja linalounganisha Crimea na Russia, litasababisha mgogoro mkubwa kwa utawala wa Ukraine.

XS
SM
MD
LG