Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 15:25

Marekani: Maafisa wahofia habari potofu zinaweza kuchochea ghasia katika uchaguzi


Rais wa Russia Vladimir Putin
Rais wa Russia Vladimir Putin

Ikiwa  imebakia wiki moja kwa uchaguzi wa katikati ya muhula wa Marekani, afisa wa ngazi ya juu wa Marekani ameeleza wasiwasi kuwa habari potofu, au operesheni za ushawishi zinazofanywa na  maadui  wa kisiasa Marekani, zinaweza kuchochea ghasia katika upigaji kura.

Kwa wiki kadhaa, maafisa wa ngazi ya juu kutoka Idara ya ya Upelelezi ya serikali kuu na Wizara ya Usalama wa Ndani zimesema hazijagundua dalili mahsusi au uhakika wa vitisho kwa upigaji kura wa Novemba 8.

Lakini maafisa wameeleza hofu yao zaidi kuhusu mivutano ya ndani ya kisiasa inayoongezeka ambayo imeenea sehemu kubwa ya nchi na vipi hilo linaweza kujitokeza katika siku ya uchaguzi iwapo itachanganyika na uongo na maelezo ya kupotosha, wakati mwengine kutoka katika mataifa ya kigeni kama vile Russia, China na Iran.

“Ni wasiwasi mkubwa sana,” Jen Easterly, mkurugenzi wa Shirika la Usalama wa Mitandao Marekani na Usalama wa Miundombinu(CISA) ameuambia mkutano mmoja Jumanne huko Washington. “ Umepata taarifa potofu, ambazo zinaweza kutumiwa na maadui wa nje kupandikiza chuki kati ya wa Marekani ili kuharibu ari ya heshima ya chaguzi zetu mbalimbali na kuchochea ghasia dhidi ya maafisa wa uchaguzi.”

FILE - Jen Easterly, Iowa, Aug. 14, 2021.
FILE - Jen Easterly, Iowa, Aug. 14, 2021.

Kwa kuongezea “unashuhudia wasiwasi unaokera wa usalama wa maeneo kwa kiwango ambacho hakijawahi kushuhudiwa, hofu ya vitisho, ghasia, kubughudhiwa kwa maafisa wa uchaguzi, maeneo ya kupiga kura, wapiga kura,” alisema.

CISA, ambayo inahusika kama shirika linaloongoza usimamizi wa uchukuaji tahadhari juu ya usalama wa chaguzi, haliko peke yake katika kueleza wasiwasi huu.

Wafuasi wa Rais wa zamani Donald Trump wakikabiliana na vikosi vya polisi na usalama wakati walipovamia Bunge la Marekani huko Capitol Hill, Washington, DC, Januari 6, 2021.
Wafuasi wa Rais wa zamani Donald Trump wakikabiliana na vikosi vya polisi na usalama wakati walipovamia Bunge la Marekani huko Capitol Hill, Washington, DC, Januari 6, 2021.

Wizara ya Usalama wa Ndani (DHS) imerejea kuonya kuhusu uwezekano wa kutokea ghasia wakati wa uchaguzi wa katikati ya muhula, wakieleza huko nyuma mwezi Juni kuwa uchaguzi unaweza kugeuka kuwa eneo la mkusanyiko wenye misimamo mikali ya kisiasa ndani ya nchi ikilenga kuleta ghasia.

Na maafisa wa polisi wao vilevile wametahadharisha kuwa idadi ya vitisho dhidi ya wafanyakazi wa uchaguzi na maafisa wa uchaguzi vimeongezeka zaidi, huku kukiwepo zaidi ya ripoti 1,000 juu ya hilo tangu mwezi Juni 2021.

Kati ya hizo ripoti, takriban asilimia 60 zimewasilishwa kutoka majimbo saba, yote hayo yameshuhudia matokeo ya uchaguzi wa urais wa Marekani wa 2020 ukipingwa na wenye kukanusha ushindi au kuchunguzwa kwa sababu ya madai yasiyokuwa na ushahidi ya wizi wa kura.

XS
SM
MD
LG