Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 04:47

Kenya na Marekani zinataka mzozo wa Ethiopia kutatuliwa haraka iwezekanavyo


Mshauri wa usalama wa Marekani Jake Sullivan na mwenzake wa Kenya Dr. Monica Juma
Mshauri wa usalama wa Marekani Jake Sullivan na mwenzake wa Kenya Dr. Monica Juma

Mshauri wa usalama wa taifa wa rais wa Marekani Jake Sullivan, amefanya mazungumzo na mwenzake wa Kenya Dr. Monica Juma kuhusu vita vya Ethiopia na mgogoro wa kibinadamu unaoendelea kuongezeka nchini humo.

Sullivan, amempongeza Dr. Juma kwa kuwa wa kwanza kuteuliwa kuwa mshauri wa usalama katika historia ya Kenya.

Wawili hao wameelezea wasiwasi kutokana na kuongezeka kwa vita kaskazini mwa Ethiopia na kuitaka serikali ya Ethiopia kukubaliana na wapiganaji wa Tigray namna ya kumaliza mapigano hayo haraka iwezekanavyo.

Wawakilishi wa serikali ya Ethiopia watakutana na wawakilishi wa viongozi wa Tiagray mjini Pretoria Afrika Kusini, baadaye wiki ijayo, kwa mazungumzo ya amani.

Sullivan amesema kwamba ni muhimu kwa viongozi hao kukubaliana kusitisha vita na uhasama, kuruhusu misaada ya kibiandamu kuwafikia watu wa Tigray, wanajeshi wa Eritrea kuondoka Ethiopia na watu wote wanaohusika na ukandamizaji wa haki za kibinadamu kuwajibishwa.

Sullivan na Dr. Juma, pia wamejadiliana kuhusu hali ya ukame inayoshuhudiwa katika Pembe ya Afrika, ambapo mamilioni ya raia wa Kenya, Ethiopia na Somalia wanakabiliwa na ukosefu mkubwa wa chakula, maji na mahitaji muhimu baada ya mvua kutonyesha kwa muda mrefu.

Marekani imetoa msaada wa dola bilioni 2 mwaka huu kwa ajili ya kukabiliana na athari za ukame katika nchi zilizo Pembe ya Afrika, ikiwa ni zaidi ya nusu ya msaada wa kifedha ambao umetolewa kwa ajili ya watu wa eneo hilo kukabiliana na athari za ukame.

Marekani na Kenya zimekubaliana kuendelea kuimarisha uhusiano wao na kuahidi ushirikiano thabithi katika kutatua changamoto zinazolikumba eneo hilo na dunia kwa jumla.

XS
SM
MD
LG