Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 21:09

FAO : Watu zaidi ya milioni 4 waathirika vibaya na ukame Kenya


Wakazi wa Wajir wakisubiri maji.
Wakazi wa Wajir wakisubiri maji.

Watu zaidi ya milioni 4 wameathirika vibaya na ukame nchini Kenya kwa mujibu wa shirika la Chakula la FAO.

Maelfu ya watoto wanahangaika kupata lishe ikiwa baadhi ya wanafunzi wakilazimika kuacha shule kutokana na makali ya njaa.

MATUKIO YA AFRIKA ATHARI YA UKAME WAJIR GARISSA.mp3
please wait

No media source currently available

0:00 0:05:09 0:00

Katika Kaunti za kaskazini mashariki mwa Kenya athari ya ukame inazidi kuleta maafa makubwa huku watoto wadogo wakipata utapia mlo. Mwandishi wetu wa Nairobi alitembeela Kaunti za Kaskazini Mwa Kenya na kushuhudia hali halisi.

Katika Hospitali ya Wajir Kaskazini Mashariki mwa Kenya…. Idadi ya watoto walioathirika na utapia mlo unazidi kuongezeka kutokana na makali ya ukame unaozidi kubisha hodi.

Wakazi wa Garissa wakiwa katika eneo la makazi yao.
Wakazi wa Garissa wakiwa katika eneo la makazi yao.

Hali hii huenda ikawa mbaya Zaidi iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa . Waathiriwa wakiwa ni wanawake na watoto walio chini ya miaka mitano.

Mwanawe mama Fatuma ameugua kwa muda kutokana na Utapia mlo … anahofia huenda hali ya mwanawe ikawa mbaya Zaidi.

Watoto Zaidi ya 30 wameathirika maeneo ya Garissa, wajir n ahata mandera . Ukame ya muda mrefu uimelazimisha familia kuondoka majumbani mwao kutafuta chakula na maji, na hivyo kuhatarisha afya zao, usalama na elimu.

Katra Farah Mtaalam wa Lishe katika shirika la Save the Children anasema imekuwa vigumu kwa familia nyingi huku baadhi yao wakilala njaa au kupata mlo moja kwa siku.

Mtaalam wa Lishe Katra Farah katika eneo la Wajir.
Mtaalam wa Lishe Katra Farah katika eneo la Wajir.

Mwaka huu sehemu kame zilipokea mvua kwa kiwango cha cha chini Zaidi kuwahi kushuhudiwa na kuathiri sana uzalishaji wa mimea na vyakula vya mifugo.

Mwanamazingira kaunti ya Garissa Abdikadir Aden anahoji kuwa huu ni wakati wa jamii kuelemishwa kuhusu mabadailiko ya hali ya anga ilikujitayarisha na kuangazia suala hilo.

Kwa misimu minne iliyopita ya mvua, mvua za kila mwaka hazikuweza kunyesha kote nchini Kenya, Ethiopia na Somalia na kuwalazimu watu milioni 1.5 kukimbia makazi yao kutafuta chakula na maji kwingineko.

Mwanamazingira Abdikadir akiwa katika bustani ya kuotesha miti.
Mwanamazingira Abdikadir akiwa katika bustani ya kuotesha miti.

Makali ya njaa yanadhihirka wazi katika nyusio za watoto waliojaza katika vyumba vya kuimarisha hali yao hasa waliokatika hatari Zaidi

Takriban watoto milioni mbili katika Pembe ya Afrika wanahitaji matibabu ya haraka kwa utapiamlo unaotishia maisha, kulingana na makadirio ya Save the children.

Athari za ukame katika eneo la Wajir, Kenya.
Athari za ukame katika eneo la Wajir, Kenya.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Kuratibu Masuala ya Kibinadamu inakadiria watu milioni 7.8 nchini Somalia wameathiriwa na ukame, ikiwa ni pamoja na zaidi ya 1.1. mamilioni ya watu waliokimbia makazi yao.

Shirika la OCHA linakadiria kati ya sasa na Desemba ikiwa misaada ya kibinadamu haitawafikia watu wanaohitaji Zaidi basi matokeo huneda yakawa maafa Zaidi . Kufikia sasa, asilimia 45 ya usaidizi ya Umoja wa Mataifa ya dola bilioni 2.26 imefadhiliwa.

Imetayarishwa na mwandishi wetu Hubbah Abdi, Kenya

XS
SM
MD
LG