Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:42

Mtu mmoja kati ya watano barani Afrika anakabiliwa na njaa - UN na AU


Wakimbizi wakiwa kambini nchini Somalia ambao ni kati ya makundi yanayoathiriwa zaidi na hali ya njaa.
Wakimbizi wakiwa kambini nchini Somalia ambao ni kati ya makundi yanayoathiriwa zaidi na hali ya njaa.

Mmoja kati ya kila watu watano barani Afrika anakabiliwa na njaa, takwimu za hivi punde zaidi zinaonyesha, huku uhaba wa chakula na utapiamlo ukiongezeka katika bara hilo, maafisa wa Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa wamesema.

Mashirika hayo mawili yametaka uingiliaji kati wa haraka, huku hali ikiwa mbaya zaidi kutokana na ukame wa muda mrefu, vita barani humo, na kwingineko.

"Afŕika bila shaka inakabiliwa na mgogoŕo wa chakula unaotisha zaidi katika miongo kadhaa,” Josefa Sacko, kamishna wa AU wa Kilimo, aliuambia mkutano wa ngazi ya juu wa chakula na lishe mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Alisema kuwa janga la Covid-19 na mzozo unaoendelea kati ya Russia na Ukraine vimezidisha uhaba wa chakula na umaskini barani Afrika ikizingatiwa kuwa Russia na Ukraine ndivyo vyanzo vikuu vya ngano na alizeti kwa Afrika.

Kukosekana mvua kwa misimu minne mfululizo katika maeneo ya Ethiopia, Kenya na Somalia kunatishia kutokea baa la njaa katika jumuiya za pembe ya Afrika.

Hali hii haijawahi kushuhudiwa katika miaka 40 iliyopita ambapo mvua za chini ya wastani zimefanya maeneo ya Somalia, kusini na kusini mashariki mwa Ethiopia, na kaskazini na mashariki mwa Kenya kukabiliwa na ukame ambao umeongeza hatua za watu kuhama.

Kwa mujibu wa shirika la misaada takriban mifugo milioni 7 imekufa kote katika ukanda huo.

Shirika la watoto la Umoja wa Mataifa – UNICEF – linasema zaidi ya watoto milioni 7 wanakabiliwa na kudumaa kutokana na kukosa lishe bora.

XS
SM
MD
LG