Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 07:49

Ukosefu wa chakula unahatarisha vifo vya watoto nusu milioni Somalia


SOMALIA-SEQUÍA
SOMALIA-SEQUÍA

Idadi ya watoto wadogo wanaokabiliwa na utapiamlo sugu nchini Somalia imeongezeka na kufikia zaidi ya nusu milioni mwaka huu. Umoja wa Mataifa unasema hicho ni kiwango cha juu zaidi kuliko ilivyokuwa wakati wa njaa mwaka 2011 ambapo maelfu ya watoto walifariki.

James Elder, msemaji wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa, UNICEF, anasema kwamba kuna watoto zaidi ya nusu milioni wanaokabiliwa na kifo kinachoweza kuzuilika kutokana na ukosefu wa chakula.

Akizungumza na waandishi habari mjini Geneva Jumanne, Elder amesema kiwango hicho watoto kukabiliwa na utapiomlo hakijawahi kushuhudiwa katika karne hii wala katika nchi yoyote ile duniani.

Umoja wa Mataifa umeonya kwamba baadhi ya maeneo ya Somalia yatakumbwa na hali sugu ya njaa katika miezi ijayo wakati Pembe ya Afrika ikishuhudia msimu wa tatu mfululizo bila ya kunyesha mvua.

Njaa iliyoikumba Somalia 2011 ilisababisha zaidi ya vifo vya watu robo milioni, nusu yao wakiwa ni watoto.

Elder anasema kuna watoto laki 5 elfu 13 chini ya miaka mitano wanaotazamiwa kukabiliwa na utapiamlo ikimanisha wanaweza kufariki kutokana na magonjwa kama vile surua, malaria na kipindupindu, magonjwa yanayosambaa nchini humo hivi sasa.

Shirika la Afya Duniani WHO, wiki iliyopita lilitangaza kwamba mamia ya watu huenda wamefariki kutokana na njaa, hali ambayo inatokea chini ya miaka 10 iliyopita.

Mkuu wa WHO, Tedros Adhanom Ghebreyesus alionya kwamba sehemu kubwa ya Somalia itatumbukia katika hali ya njaa ikiwa wafadhili hawatatoa msaada unaohitajika kwa haraka iwezekanavyo.

XS
SM
MD
LG