Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 19:59

Dola bilioni moja zitahitajika ili kuepusha baa la njaa Somalia - Griffiths

Martin Griffiths, Naibu Katibu Mkuu wa Masuala ya Kibinadamu na Mratibu wa Misaada ya Dharura, akitoa maelezo kwa waandishi wa habari kuhusu njaa na hali ya kibinadamu huko Mogadishu. September 5, 2022. REUTERS/Feisal Omar.

Mkuu wa masuala  ya kibinadamu wa umoja wa Mataifa, alitabiri jumanne kwamba angalau dola bilioni moja zitahitajika haraka ili kuepusha baa la njaa nchini Somalia .

Mkuu huyo ametaja jambo hilo kutokea katika miezi ijayo na mapema mwaka ujao wakati misimu miwili zaidi ya kiangazi ambayo inatarajiwa kuingilia kati ukame wa kihistoria ambao umelikumba taifa hilo la pembe ya Afrika.

Martin Griffiths alisema katika mkutano kwa njia ya video kutoka mji mkuu wa Somalia Mogadishu, kwamba ripoti mpya kutoka kwa jopo lenye mamlaka la wataalamu huru inasema kutakuwa na baa la njaa nchini Somalia kati ya Oktoba na Disemba ikiwa hawatafanikiwa kuizuia na kuiepuka kama ilivyokuwa mwaka 2016 na mwaka 2017.

XS
SM
MD
LG