Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 04:38

UN: Njaa huenda ikatokea nchini Somalia


FILE - Watoto waliokimbia ukame katika eneo la kusini mwa Somalia wakiwa wanasubiri msaada wa chakula katika kituo cha kugawa chakula katika kambi moja Mogadishu, Somalia.
FILE - Watoto waliokimbia ukame katika eneo la kusini mwa Somalia wakiwa wanasubiri msaada wa chakula katika kituo cha kugawa chakula katika kambi moja Mogadishu, Somalia.

Umoja wa Mataifa inasema njaa nchini Somalia huenda ikatokea baadaye mwaka 2022.

Umoja wa Mataifa inasema njaa nchini Somalia huenda ikatokea baadaye mwaka huu. Mkuu wa masuala ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, Martin Griffiths, amesema kwamba kama hatua madhubuti hazitachukuliwa na jumuiya ya kimataifa kuhusu hali ya njaa ambayo duniani haijaiona kwa miaka kadhaa wataiona hali hiyo hivi sasa.

Takriban watu milioni moja nchini Somalia wamekoseshwa makazi kutokana ukame mbaya sana kuwahi kutokea kwa miongo kadhaa ambao umeathiri eneo kubwa sana la Pembe ya Afrika ikiwa ni pamoja na Ethiopia na Kenya.

Mkuu wa masuala ya kibinadamu katika Umoja wa Mataifa, Martin Griffiths alisema kwamba hali aliyoiona kwenye hospitali moja nchini Somalia katika siku za karibuni ilikuwa mbaya sana hajawahi kuiona katika muda wa miaka 50 ya kazi za kibinadamu.

“Hili halijawahi kutoka hapo kabla nchini Somalia. Kwahiyo picha zote ambazo tumekuwa nazo . Hii ni hali isiyo na kifani, ni kwasababu hiyo ndiyo maana tunapiga debe na kutikisa miti na kujaribu kupata msaada wa kimataifa katika misingi ya mtizamo, matarajio na uwezekano na khofu ya njaa inakuja Pembe ya Afrika. Hapa nchini Somalia, huenda ikawa kwanza, lakini Ethiopia na Kenya kwa hakika haziko nyuma sana,” amsema Griffiths.

Mwakilishi wa UNICEF nchini Somalia, Wafaa Saeed Abdelatef alisema kwamba “takriban nusuya watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano” huenda “wakakumbwa na utapiamlo uliokithiri.”

Aliongezea kwamba hivi sasa watu milioni nne na nusu hivi sasa wana hitaji “msaada wa dharura wa maji” hata wakati ambapo hali inatabiriwa itakuwa mbaya sana kwa msimu mwingine wa mvua, wakihofia hautaleta afueni.

Wafaa anasema"Utapiamlo umefikia viwango ambavyo havina kifani. Tuna watoto milioni moja na nusu, hii ni karibu nusu ya watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano, huenda wakakumbwa na utapiamlo uliokithiri na kati ya hao, watoto laki tatu na nusu watahitaji matibabu kwa utapiamlo mbaya sana.”

Msemaji wa UNHCR Shabia Mantoon alisema kwamba hali inavyozidi kudorora pia kuna ongezeko la wanwake na watoto kukumbwa na manyanyaso ya kijinsia kwa vile wanahitajika “kutembea mwendo mrefu sana ili kuweza kupata maji na sehemu ya kujihifadhi.”

Familia zilizokimbia ukame upande wa kusini mwa Somalia wakiwa katika kambi ya hifadhi mjini Mogadishu, Somalia, Feb. 18, 2017.
Familia zilizokimbia ukame upande wa kusini mwa Somalia wakiwa katika kambi ya hifadhi mjini Mogadishu, Somalia, Feb. 18, 2017.

Familia zenye njaa nchini Somalia zimekuwa zikitembea kwa siku kadhaa au wiki kupitia njia zenye ardhi kavu wakitafuta misaada.

Familia nyingi zimezika watu wao wakiwa njiani.

Hata wanapofika kwenye kambi nje ya maeneo ya mjini, wanakuta misaada michache au hakuna kabisa misaada. Msemaji wa UNICEF anaelezea zaidi.

"Wanawake na watoto wanalazimishwa kutembea mwendo mrefu n mbali sana kutafuta fursa za maji na makazi, wakikumbana na hatari ya manyanyaso ya kijinsia. Wakati ukame unazidi kuongezeka, wasi wasi wa ulinzi unazidi kuongezeka na hatari ya manyanyaso ya kijinsia na kingono nayo yanaongezeka pia. Watoto wengi pia wamelazimika kuacha shule kuzisaidia familia zao kupata kipato cha kila siku na. Kutafuta maji na ardhi za malisho, na kuongezeka zaidi kwa hatari za ndoa za kulazimishwa au familia kutengana," anasema shabia Mantoo.

Uhaba wa maji nchini Somalia
Uhaba wa maji nchini Somalia

Mkurugenzi wa kanda wa baraza la wakimbizi la Denmark, Audrey Crawford alisema kwamba kina mama wengi ambao amezungumza nao “wamewazika watoto wao siku za nyuma” kutokana na utapiamlo au ugonjwa.

kiasi cha watu milioni moja nchini Somalia wamekoseshwa makazi kwasababu ya ukame mbaya sana kutokea katika miongo kadhaa, na kusukumwa na mabadiliko ya hali ya hewa.

Kwa kuongezea, uvamizi wa Russia nchini Ukraine umeelezewa kama ni janga kwa Somalia, ambayo imeathiriwa sana na uhabari wa misaada wa kibinadamu wakati wafadhili wa kimataifa wakiilenga Ulaya. Audrey Crawford anafafanua zaidi.

"Zaidi ya watu milioni moja wamekoseshwa makazi ndani ya nchi hadi hivi sasa mwaka huu. wengi wao. Walitembeea kwa siku takriban kumi wakitafuta chakula na maji, waliwasili kwa hakika wakiwa hawana kitu na hali zao zimedhoofu huku watoto wakiwa na utapiamlo au watoto wao wamefariki. Kina mama wengi ambao nimezungumza nao, ama awali wamewazika watoto wao, ama kwa kuharisha au surua katika kambi ambazo zina msongamano mkubwa sana au wamekufa njiani kwasababu ya utapiamlo,” anasema Audrey Crawford.

Tangazo rasmi la njaa ni nadra na linaonya kwamba msaada mdogo sana umepatikana na umefika kwa kuchelewa.

XS
SM
MD
LG