Shambulio hilo ambalo lilianza Ijumaa jioni, lilikuwa ndilo kubwa zaidi kukumba mji mkuu wa Somalia tangu Mohamud aingie madarakani mwezi Juni na kusisitiza changamoto ya kujaribu kumaliza uasi wa miaka 15 wa kundi lenye uhusiano na Al-Qeada.
Watu 21 walifariki na wengine 117 kujeruhiwa katika shambulio hilo la bunduki na mabomu lililolenga hoteli maarufu ya Hayat, na raia wa Norway ni miongoni mwa waliokufa, kwa mujibu wa serikali ya Norway.
“Ninajua kwamba wanainchi wa Somalia wamechoshwa na rambirambi na maombolezo yasiyoisha, najua kwamba mnawapoteza watu wenye thamani katika kila shambulio linolafanywa na magaidi,” Mohamud amesema.
“Tuna dhamira ya kuwadhoofisha magaidi wanaoteketeza wanainchi wetu hadi maeneo yote wanayoyadhibiti yamekombolewa, hili ni jambo la kipaumbele kwa serikali yetu na maandalizi na utelekelezaji wa mpango huo unaendelea,” amesema bila kufafanua zaidi.