Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 02:55

Takriban watu 20 wauwawa kwenye shambulizi la kigaidi Somalia


Hoteli ya Hayat iliyoshambuliwa na magaidi mwishoni mwa wiki Mogadishu
Hoteli ya Hayat iliyoshambuliwa na magaidi mwishoni mwa wiki Mogadishu

Polisi wa serikali kuu ya Somalia wamesema Jumapili kwamba maafisa wa usalama wamemaliza kushikiliwa kwa  hoteli moja kwenye mji mkuu wa Mogadishu. 

Shambulizi hilo lilifanywa na kundi la wanamgambo la al Shabab lenye uhusiano na kundi la al Qaida, baada ya operesheni iliyochukua karibu saa 30. Ripoti zimeongeza kwamba zaidi ya watu 20 waliuwawa wakati wa tukio hilo la mwishoni mwa wiki.

Wakati akizungumza mbele ya wanahabari mjini mogadishu, mkuu wa polisi nchini generali Abdi Hassan Hijar alisema kwamba miongoni mwa watu waliokufa ni raia wa kawaida, pamoja na maafisa wa usalama, baada ya shambulizi kwenye hoteli ya Hayat, iliyoko kati kati ya mji , karibu na makao makuu ya idara ya uchunguzi wa kihalifu.

Amesema jukumu kubwa la maafisa wake lilikuwa kuwaokoa watu waliokwama ndani baada ya wapiganaji wa al Shabab kuishambulia hoteli hiyo kwa vilipuzi, na kulivamia jengo hilo ambapo mapambano ya risasi yalifuatia na kudumu kwa karibu saa 30.

Ameongeza kusema kwamba maafisa waliohusika kwenye operesheni hiyo iliyomalizika usiku wa manane waliwaokoa zaidi ya watu 106, wakiwemo wanawake na watoto.

XS
SM
MD
LG