Upatikanaji viungo

Breaking News
Ijumaa, Oktoba 18, 2024 Local time: 06:15

Watu zaidi ya milioni 37 wanataabika na njaa katika Pembe ya Afrika-Mashirika ya misaada


 Kadija Mohamed akiwapikia watoto wake chakula katika kambi iliyowekwa kwa ajili ya wakimbizi wa ndani huko Dinsoor, Januari 5, 2012.SOMALIA
Kadija Mohamed akiwapikia watoto wake chakula katika kambi iliyowekwa kwa ajili ya wakimbizi wa ndani huko Dinsoor, Januari 5, 2012.SOMALIA

Makundi ya misaada yanasema zaidi ya watu milioni 37 katika Pembe ya Afrika wanataabika na njaa ambayo imechochewa na ukame mbaya sana, ambao umeua takriban wanyama milioni 9.

Makundi ya misaada yanasema zaidi ya watu milioni 37 katika Pembe ya Afrika wanataabika na njaa ambayo imechochewa na ukame mbaya sana, ambao umeua takriban wanyama milioni 9.

Hali mbaya sana inasadikiwa iko nchini Somalia, ambako zaidi ya watoto 700 wamefariki kwa utapiamlo mwaka huu.

Ikichangiwa na matokeo ya janga la Covid 19 na vita vya Russia nchini Ukraine, hali ya njaa ulimwenguni inazidi kuwa mbaya zaidi siku hadi siku, kwa mujibu wa watalaamu.

Dr. Deepmala Mahla ni makamu rais wa masuala ya kibinadamu katika shirika la CARE International.

Dr. Deepmala Mahla anasema “dunia inakabiliwa na athari mbaya sana za mzozo wa njaa ulimwenguni, na hili linatokea katika dunia yenye vitu vingi. Sisi tunazungumzia kuhusu watu milioni 50 ambao wako hatua moja tu kukumbwa na njaa.”

Mzozo umekuwa hasa katika eneo lenye shida la Pembe ya Afrika, ambalo linakabiliana na msimu wa tano mfululizo wa mvua zilizofeli na vipindi virefu vya ukame ambavyo vilianza Oktoba mwaka 2020.

Nchini Ethiopia, Kenya na Somalia, zaidi ya watu milioni 36 wanakabiliana na njaa sugu, kwa mujibu wa CARE International.

Nchini Somalia peke yake, zaidi ya watoto 700 wamefariki kwa utapiamlo mwaka huu na watalaamu wanasema mzozo wa kibinadamu utazidi kufanya hali kuwa mbaya sana katika miezi ijayo wakati njaa tayari imetabiriwa katika mikoa miwili ya nchi hiyo.

Alinur Aden ni mkurugenzi mtendaji wa Gargaar Relief and Development Organization (GREDO), taasisi ya kibinadamu nchini Somalia.

Aden anasema “janga la Covid 19, mabadiliko ya hali ya hewa, uvamizi wa nzige na misimu minne mfululizo ya mvua ambazo hazikuwa za kawaida vimechangia kwa matatizo yote haya.”

Wanawake na watoto wanabeba mzigo wa njaa. Kwa mujibu wa Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, watoto 942,000 walio na umri wa chini ya miaka mitano na wanawake wajawazito 135,000 na wale wanaonyonyesha wana utapiamlo mbaya sana na wanahitaji matibabu katika mikoa yenye hali ya ukavu ambayo imekumbwa na ukame nchini Kenya.

Abyan Ahmed ni mshauri wa masuala ya kibinadamu yanayohusu lishe katika shirika la CARE, anasema “tayari tunaona viwango vya kutisha vya vifo na utapiamlo vikitokea katika nchi zote tatu.

Tumeona ongezeko la viwango kote katika nchi hizo katika robo ya kwanza yam waka 2022, na idadi ya kesi mbaya sana imeongezeka mpaka kufikia 15% katika miezi mitano iliyopita, ambapo kimsingi ina maana kwamba katika kila dakika, mtoto mmoja zaidi anakumbwa na ukowefu wa lishe na kuna hatari inayoongezeka ya kufariki ikiwa hakuna uingiliaji kati.”

Dr. Mahla anasema uingiliaji wa haraka sana unahitajika. “Kwa hiyo, tunawataka viongozi wa dunia, jamii ya kimataifa, serikali, kufanya juhudi. Kutenga haraka sana, rasilimali kila mwaka ili tuweze kutoa majibu ya kibinadamu kuwasaidia watu hivi sasa kwasababu katika Pembe ya Afrika wanahitaji kwa sisi kuchukua hatua hivi sasa na siyo baadaye,” ameongezea.

Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa limetoa takriban dola bilioni 1.3 za misaada kwa ajili ya misaada ya kibinadamu katika Pembe ya Afrika tangu mwaka 2020.

Wakati wa hotuba yake kwenye Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa wiki hii, Rais Joe Biden aliahidi dola bilioni 10 kupambana na njaa ulimwenguni, lakini bado haiko bayana kiasi gani kitakwenda Pembe ya Afrika.

XS
SM
MD
LG