Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatatu, Desemba 23, 2024 Local time: 23:01

Sudan yakabiliwa na mzozo wa kibinadamu-Mashirika ya Umoja wa Mataifa


Nyumba zimeharibika baada ya mvua kubwa kunyesha katika kijiji cha Aboud katika wilaya ya El-Manaqil katika mkoa wa Al-Jazirah, kusini mashariki mwa Khartoum, Sudan, Jumanne, Agosti 23, 2022.(AP Photo/Marwan Ali).
Nyumba zimeharibika baada ya mvua kubwa kunyesha katika kijiji cha Aboud katika wilaya ya El-Manaqil katika mkoa wa Al-Jazirah, kusini mashariki mwa Khartoum, Sudan, Jumanne, Agosti 23, 2022.(AP Photo/Marwan Ali).

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaonya kuwa Sudan inakabiliwa na mzozo wa kibinadamu ambao haukutarajiwa kwasababu ya mavuno duni, kupanda kwa bei za mafuta, ukosefu wa uthabiti wa kisiasa na ukosefu wa misaada wa kifedha.

Karibu theluthi moja ya Sudan yenye takriban watu milioni 45 haina chakula cha kutosha cha kula. Shirika la Mpango wa Chakula Duniani (WFP), linaonya kuwa idadi ya watu wenye njaa huenda ikaongezeka mpaka milioni 18 ifikapo mwisho wa mwezi kama wafadhili hawatajitokeza kutoa fedha ili kuwalisha.

Mwakilishi wa WFP nchini Sudan na mkurugenzi wa kanda Eddie Rowe anasema uagizaji kutoka nje wa Sudan ni kiasi cha asilimia 80 ya ngano yake inatoka Ukraine. Anasema vita nchini Ukraine vimesababisha kupanda kwa bei ya chakula, mafuta na bidhaa nyingine za msingi. Anasema vita pia vinafanya iwe vigumu zaidi kupata fedha zinazohitajika kwa operesheni za kibinadamu.

Anasema WFP haina fedha na imelazimika kupunguza mgao wa chakula kwa nusu kwa ajili ya watu milioni 2.4 nchini Sudan. Hii inajumuisha wakimbizi 600,000 ambao kwa jumla wanategemea misaada ya kimataifa. Anasema hali mbaya zaidi inatarajiwa kutokea.

Rowe anasema “tuko katika hali ya kusimamisha kwa muda au kusitisha kabisa harakati muhimu. Kwa mfano, tunapanga kuwafikia wanafunzi milioni mbili kwa kuwapatia chakula shuleni, na hili linaonekana kuwa ni ukweli ambao si rahisi kuufikia kutokana na kwamba hatua ufadhili.”

Mwakilishi wa UNICEF nchini Sudan, Mandeep O’Brien, anasema Sudan inakabiliwa na mzozo wa utapiamlo pamoja na mzozo wa njaa.

O’Brien anasema watoto milioni tatu walio na umri wa chini ya miaka mitano wana utapiamlo uliokithiri nchini Sudan.. Hivi tunavyozungumza, watoto 650,000 wanataabishwa na utapiamlo mbaya sana uliokithiri. Kama hawatapatiwa matibabu, nusu yao watafariki.”

Anaelezea kuwa maelfu ya watoto wameshindwa kupatiwa chanjo za kuokoa maisha kwa sababu ya janga la Covid 19 na milioni saba hawako shule.

Mashirika ya Umoja wa Mataifa yanaonya. Kuwa muda wa kutoa misaada ya kuokoa maisha kwa watu milioni 10.9 walio katika mazingira hatarishi unakwenda mbio. Wanaelezea kuwa 36% ya dola bilioni 1.9 za Umoja wa Mataifa kwa Mpango wa Majibu ndiyo zimetolewa kwa mwaka huu.

XS
SM
MD
LG