Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 08:33

Marekani yawawekea vikwazo viongozi wa Al Shabab


Wizara ya Fedha ya Marekani mjini Washington ilisema kwamba imewawekea vikwazo kundi la wanachama wa ngazi za juu wa kundi la wanamgambo wa al-Shabab lenye makao yake Somalia.
Wizara ya Fedha ya Marekani mjini Washington ilisema kwamba imewawekea vikwazo kundi la wanachama wa ngazi za juu wa kundi la wanamgambo wa al-Shabab lenye makao yake Somalia.

Marekani inapanua mapambano yake dhidi ya washirika wa al-Qaida nchini Somalia, na kuongeza awamu mpya ya vikwazo vya mashambulizi ya ndege zisizo na rubani na ushauri wa kijeshi kutoka kwa vikosi vya Marekani ardhini.

Wizara ya Fedha Jumatatu ilifichua vikwazo vilivyowalenga viongozi wanne wakuu wa al-Shabab pamoja na watendaji sita, wote wanaosemekana kuwa wahusika wakuu katika mtandao unaoshtakiwa kwa kuchangisha fedha, kuajiri wapiganaji na kununua silaha.

Kulingana na Marekani, mtandao wa magendo ulichukua fedha kutoka kwenye vyanzo mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali, kusaidia al-Shabab kuzalisha wastani wa dola milioni 100 kwa mwaka, na kusaidia kukuza ukubwa na uwezo wa kundi hilo la kigaidi.

Ripoti ya mapema mwaka huu ya taasisi ya usalama yenye makao yake mjini Mogadishu, Taasisi ya Hiraal iliyothibitishwa baadaye na makadirio ya kijasusi yaliyotolewa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa inaonyesha takriban robo ya fedha hizo, au kiasi cha dola milioni 24, zinatumika kwa silaha pekee.

XS
SM
MD
LG