Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 03:58

Rais wa Somalia asema waliouwawa katika milipuko wafikia takriban 100


Watu wakiangalia uharibifu uliofanywa na magari mawili yaliyokuwa yametegwa mabomu kwenye makutano yenye shughuli nyingi huko Mogadishu, Somalia, Jumapili, Oktoba 30, 2022. (AP)
Watu wakiangalia uharibifu uliofanywa na magari mawili yaliyokuwa yametegwa mabomu kwenye makutano yenye shughuli nyingi huko Mogadishu, Somalia, Jumapili, Oktoba 30, 2022. (AP)

Idadi ya watu waliouwa katika katika milipuko miwili ya magari kwenye makutano yenye shughuli nyingi katika mji mkuu wa Somalia imefikia takriban 100.

Hayo ni kwa mujibu wa Rais wa Somalia, na idadi hiyo inaweza kuongezeka kufuatia shambulio hilo baya zaidi nchini humo tangu shambulio la lori katika eneo hilo hilo miaka mitano iliyopita na kuuwa zaidi ya watu 500.

Rais Hassan Sheikh Mohamud, akiwa katika eneo la milipuko ya Jumamosi huko Mogadishu, aliwaambia waandishi wa habari kwamba karibu watu wengine 300 walijeruhiwa. "Tunawaomba washirika wetu wa kimataifa na Waislamu duniani kote kutuma madaktari wao hapa kwani hatuwezi kuwapeleka waathiriwa wote nje ya nchi kwa matibabu," alisema.

Kundi la al-Shabab lenye uhusiano na al-Qaida, ambalo mara nyingi hulenga mji mkuu na kudhibiti maeneo makubwa ya nchi, lilidai kuhusika, likisema lengo lake lilikuwa kulipua wizara ya elimu. Ilidai kuwa wizara hiyo ni "ngome ya maadui" ambayo hupokea usaidizi kutoka kwa nchi zisizo za Kiislamu na "imejitolea kuwaondoa watoto wa Kisomali kutoka kwenye imani ya Kiislamu."

Wakati huo huo mshauri wa usalama wa taifa wa Ikulu ya Marekani Jake Sullivan alisema Jumapili kwamba Marekani "inalaani vikali shambulio hilo la kigaidi" huko Mogadishu, ambapo mabomu yaliyotegwa kwenye gari yalilipuka katika wizara ya elimu ya Somalia karibu na soko lenye shughuli nyingi.

XS
SM
MD
LG