Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 08:31

Idadi ya watu waliouawa na mabomu Somalia imeongezeka na kufikia 120


Watu wakiangalia uharibifu ulioachwa na magari mawili yaliyokuwa yametegwa mabomu kwenye makutano yenye shughuli nyingi huko Mogadishu, Somalia, Jumapili, Oktoba 30, 2022.(AP)
Watu wakiangalia uharibifu ulioachwa na magari mawili yaliyokuwa yametegwa mabomu kwenye makutano yenye shughuli nyingi huko Mogadishu, Somalia, Jumapili, Oktoba 30, 2022.(AP)

Idadi ya watu waliouawa na mabomu mawili ya kwenye gari yaliyolipuka nje ya wizara ya elimu katika mji mkuu wa Somalia Mogadishu imeongezeka na kufikia watu 120, waziri wa afya alisema siku ya Jumatatu.

Kundi la al-Shabaab lenye uhusiano na al-Qaeda lilidai kuhusika na milipuko hiyo ya Jumamosi, ambayo ni mibaya zaidi kuwahi kutokea nchini Somalia tangu kutokea kwa bomu la kwenye lori kuua zaidi ya watu 500 katika eneo hilo hilo miaka mitano iliyopita.

Mlipuko wa kwanza ulipiga wizara ya elimu mwendo wa saa mbili usiku. Jumamosi. Mlipuko wa pili ulipiga dakika chache baadaye wakati gari la wagonjwa lilifika na watu walikusanyika kusaidia waathiriwa.

Waziri wa afya Ali Haji Aden alisema idadi ya waliofariki ilifikia 120, huku watu wengine 150 wakitibiwa hospitalini.

Al Shabaab, ambao wanataka kuiangusha serikali na kuanzisha utawala wao wenyewe kwa kuzingatia tafsiri kali ya sheria za Kiislamu, mara nyingi hufanya mashambulizi mjini Mogadishu na kwingineko.

XS
SM
MD
LG