Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumamosi, Novemba 23, 2024 Local time: 08:00

Milipuko miwili ya mabomu yaitikisa tena Somalia

Mfano wa milipuko iliyotokea miaka iliyopita katika mji mkuu wa somalia, Mogadishu
Mfano wa milipuko iliyotokea miaka iliyopita katika mji mkuu wa somalia, Mogadishu

Kundi la Kiislamu la Al Shabaab mara nyingi hufanya mashambulizi ya mabomu na bunduki mjini Mogadishu na kwingineko, lakini haikufahamika iwapo lilihusika na milipuko ya karibuni.

Milipuko miwili ya bomu yaliyotegwa kwenye gari katika wizara ya elimu ya Somalia iliutikisa mji mkuu Mogadishu siku ya Jumamosi na kulipua madirisha ya majengo yaliyo karibu, mashahidi na huduma za dharura walisema.

Kundi la Kiislamu la Al Shabaab mara nyingi hufanya mashambulizi ya mabomu na bunduki mjini Mogadishu na kwingineko, lakini haikufahamika iwapo lilihusika na milipuko ya karibuni.

"Mabomu mawili yaliyotegwa kwenye gari yalilenga jengo la wizara ya elimu pamona na barabara ya K5," mkazi Ahmed Nur aliliambia shirika la habari la Reuters.

Mlipuko wa kwanza ulipiga kuta za wizara hiyo wakati mlipuko wa pili ulitokea wakati magari ya kubebea wagonjwa yalipowasili na watu kukusanyika kuwasaidia waathirika, kapteni wa polisi Nur Farah ameliambia shirika la habari la Reuters.

"Mlipuko wa pili uliteketeza gari letu la wagonjwa tulipofika kuwasafirisha majeruhi wa mlipuko wa kwanza," Abdikadir Abdirahman, mwanzilishi wa huduma za magari ya kubeba wagonjwa ya Aamin aliliambia shirika la habari la Reuters, akiongeza dereva na mfanyakazi wa huduma ya kwanza wamejeruhiwa katika mlipuko huo.

Alisema bado hawajui iwapo kulikuwa na vifo vyovyote au ni watu wangapi wamejeruhiwa katika milipuko yote miwili.

XS
SM
MD
LG