Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Desemba 24, 2024 Local time: 01:58

Al-Shabaab wamelipua gari na kushambulia hoteli kwa risasi Kisimayu


Gari lililoharibiwa kutokana na shambulizi la kundi la kigaidi la al-shabaab
Gari lililoharibiwa kutokana na shambulizi la kundi la kigaidi la al-shabaab

Watu watatu wameuawa kufuatia mlipuko wa bomu la kutegwa kwenye gari, Pamoja na shambulizi la bunduki katika hoteli mjini Kisimayo, nchini Somalia.

Polisi wamesema kwamba mashambulizi ya risasi yameanza baada lililokuwa limebeba mabomu kugonga lango kuu la hoteli ya Tawakal.

Kundi la kigaidi la al-shabaab lenye uhusiani na Al-Qaenda limedai kuhusika na shambulizi hilo.

Watu 8 wamejeruhiwa na wanatibiwa katika hospitali ya Kismayu.

Televisheni ya serikali ya Somalia imeripoti kwamba maafisa wa usalama wanakabiliana na hali katika sehemu hiyo.

Kuna ripoti kwamba shambulizi hilo limetokea wakati kulikuwa na mkutano wa maafisa wa usalama kwenye hoteli hiyo, namna ya kukabiliana na kundi la kigaidi la al-shabaab.

Video zilizopeperushwa na televisheni ya taifa zinaonyesha maafisa wa usalama wakisaidia watu waliojeruhiwa.

Msemaji wa kundi la kigaidi la al-Shabaab Abdiasis Abu Musab, amesema kwamba kundi hilo ndilo limetekeleza shambulizi, na kwamba lililenga wakuu wa Jubbaland, ambao hufanya kazi yao wakiwa katika hoteli ya Tawakal.

Naibu mkuu wa polisi wa Jubbaland Mohamed Nasi Guled, amesema kwamba shambulizi limetekelezwa na watu watatu.

Kismayu ni mji mkuu wa kibishara wa Jubbaland, kusini mwa Somalia. Unadhibitiwa na wapiganaji wa al-Shabaab.

Kundi hilo lilifukuzwa kutoka Kisimayu mnamo mwaka 2012. Mji huo ni muhimu kwa mapato ya kifedha kuendesha shughuli za al-shabaab, kutoka kwa uuzaji wa mkaa, na biashara ya magendo.

Shambulizi la mwaka 2019 dhidi ya hoteli mjini Kisimayu liliua watu 26.

XS
SM
MD
LG