Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 10:54

Rais wa Somalia anaomba msaada wa kimataifa kufuatia shambulizi nchini mwake


Shambulizi la Jumamosi katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu
Shambulizi la Jumamosi katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu

Tunatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa, ndugu wa Somalia, na ndugu wengine wa Kiislamu pamoja na washirika kupeleka madaktari Somalia kwenye hospitali kuwasaidia kuwatibu watu waliojeruhiwa," Rais Hassan Sheikh Mohamud alisema

Magari makubwa ya taka yalikuwa bado yanasafisha eneo la mlipuko katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu siku ya Jumatatu wakitafuta miili inayohofiwa kukwama chini ya kifusi.

Shambulizi la Jumamosi, ambalo pia lilijeruhi zaidi ya watu 300 lilidaiwa kufanywa na kundi la jihadi la Al-Shabaab na lilikuwa baya zaidi katika taifa hilo tete la Pembe ya Afrika katika kipindi cha miaka mitano.

"Tunatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa, ndugu wa Somalia, na ndugu wengine wa Kiislamu pamoja na washirika kupeleka madaktari Somalia kwenye hospitali kuwasaidia kuwatibu watu waliojeruhiwa," Rais Hassan Sheikh Mohamud alisema katika taarifa siku ya Jumapili.

Alionya kuwa idadi ya vifo huenda ikaongezeka, kwani hospitali zenye wagonjwa pia zimeharibiwa.

Somalia imekumbwa na machafuko tangu kuanguka kwa utawala wa kijeshi wa rais Siad Barre mwaka 1991 na ina moja ya mifumo dhaifu zaidi ya afya duniani baada ya miongo kadhaa ya mzozo.

"Hatuwezi kuwasafirisha kwa ndege idadi yote hii ya watu waliojeruhiwa. Hivyo yeyote anayeweza kututumia msaada tunaomba afanye hivyo," alisema Mohamud.

Waziri Mkuu Hamza Abdi Barre ameagiza shule kufungwa ili wanafunzi waweze kushiriki katika harakati za kitaifa za kuchangia damu.

Shirika la afya duniani WHO limesema liko tayari kuisaidia serikali kuwahudumia majeruhi na kutoa huduma za wale wanaopata kiwewe.

XS
SM
MD
LG