Polisi na walioshuhudia tukio hilo wametoa madai kuwa watu hao waliouawa walikuwa na nia ya kufanya mashambulizi katika jimbo la kaskazini magharibi la Bubanza.
Watu hao kutoka nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) waliingia jimboni humo Jumanne alfajiri na waliuawa katika wilaya ya Musigat msemaji wa polisi Moise Nkurunziza alisema katika radio ya serikali ya nchi hiyo, RTNB.
Kundi hilo lilikuwa na nia ya kurudia mauaji ya Ruhagarika, akiwa na maana shambulizi lililofanywa mwaka 2018, ambalo liliuwa watu wapatao 26.
Shambulizi hilo lilitokea siku chache kabla ya kura ya maoni ya katiba ambayo ilibadilishwa na kufungua njia kwa Rais Pierre Nkrunzinza kusalia madarakani mpaka mwaka 2034.
Hata hivyo, nkurunziza amesema hatawania urais katika uchaguzi wa mwakani.