Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumanne, Novemba 05, 2024 Local time: 13:47

Baraza la Seneti Marekani : Serikali ya Tanzania inaminya haki za binadamu, demokrasia


Rais John Magufuli alipokutana na ujumbe wa Benki ya Dunia nchini Tanzania.
Rais John Magufuli alipokutana na ujumbe wa Benki ya Dunia nchini Tanzania.

Maseneta wa Marekani wamemuandikia barua Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Mike Pompeo wakieleza wasiwasi wao juu kushuka kwa kuheshimiwa kwa haki za binadamu na demokrasia nchini Tanzania.

Maseneta hao wasema: "Tangu mwaka 2015 nchi hiyo inaongozwa kwa sera zinazotengeneza mazingira ya uvunjifu wa amani, vitisho na ubaguzi.

Haki za binadamu

Wamedai katika barua iliyotumwa Desemba 12, Serikali inaminya haki za binadamu na demokrasia. Wameongeza kuwa tangu mwaka 2016 nchi hiyo haina Balozi rasmi nchini Tanzania hivyo ni lazima Balozi ateuliwe.

Maseneta wanataka ubalozi wao uanze kufanya juhudi za kuhakikisha kunakuwa na uchaguzi huru na wa haki mwaka 2020.

Pia wameitaka Marekani ihakikishe hakuna fedha zinazotolewa na taasisi yoyote ya kimataifa kufadhili sera zinazoonekana kuwa kinyume na haki za binadamu.

“Tunakuandikia tukiwa na wasiwasi mkubwa juu ya kuminywa kwa uhuru wa kisiasa Tanzania, na tunahimiza uongozi wa Marekani kuongeza mawasiliano kuonyesha ongezeko la mmomonyoko wa haki za raia na uhuru wa kidemokrasia katika nchi hiyo.

Uongozi wa Magufuli

Tangu uongozi wa Rais John Magufuli uchukue madaraka mwaka 2015, umekuwa ukiendeshwa na sera za kutumia mabavu, na vitendo vya uvunjifu wa amani na vitisho dhidi ya jumuiya za kiraia, vyombo vya habari na vyama vya upinzani.

Barua hiyo imeandika pia wasichana wanalazimishwa kupimwa mimba; wale walio wajawazito wanafukuzwa na kuzuiliwa kumaliza masomo yao.

Imeeleza kuwa Rais Magufuli amezuia ufadhili wa Marekani wa programu ya HIV/AIDS iliyokuwa inawafikia na kutoa huduma ya afya kwa mashoga, idadi muhimu ya watu wanaolengwa na jitihada za kupambana na HIV/AIDS.

Vyombo vya habari

Barua hiyo imesema kuwa Magazeti yamekuwa yakidhibitiwa kwa kutozwa faini au kufungiwa kwa kuripoti habari ambazo zinaonekana kuikosoa serikali.

Sheria ambazo zinaminya uhuru wa vyombo vya habari na kuzuia maudhui kwenye mitandao ya jamii zimepitishwa kuwa sheria, zote hizo wakati wa utawala wa Magufuli.

Viongozi wa upinzani

Viongozi wa upinzani bungeni wamepigwa risasi baada ya kumkosoa Rais, wamekamatwa na kubughudhiwa na polisi, na wengine wameshtakiwa kwa makosa ya uchochezi.

Barua hiyo inaelelza hatua za wadau katika jumuiya ya kidiplomasia walizochukuwa kukabiliana na kutetereka kwa demokrasia na kuzuka kwa vitendo vya ubaguzi.

Umoja wa Ulaya

Tayari Umoja wa Ulaya umemwita Balozi wake kutoka Tanzania baada ya kile kilichoitwa ni ‘kulazimishwa kuondoka’ kutoka Tanzania, na msaada wake wa kifedha na sera zake kwa Tanzania zinajadiliwa.

Serikali ya Denmark

Mfadhili mwengine muhimu, Denmark, amesema itazuia msaada wa kifedha wenye thamani dola za Marekani milioni 10, ikieleza wasiwasi wake juu ya uvunjifu wa haki za binadamu na “kauli za sheria kali na vitisho zisizo kubalika dhidi ya wapenzi wa jinsia moja” zilizotolewa na maafisa wa serikali.

Benki ya Dunia

Benki ya Dunia ilikuwa tayari imezuia ujumbe wake kwenda Tanzania, na kusema itaruhusu ujumbe huo kuzuru nchi hiyo iwapo tu serikali itawahakikisia kuwa itajizuilia na kuwabughudhi na kuwabagua watu kutokana na mwenendo wa jinsia zao.

Benki hiyo imetishia kufuta mpango wa mkopo wa dola za Marekani milioni 300 ziilizotengwa kwa ajili ya Tanzania baada ya nchi hiyo kurejea tena msisitizo wa sera yake ya kuwapiga marufuku wasichana wenye mimba kurudi shuleni na imefanya ni kosa la jinai “kuhoji takwimu rasmi” za serikali hadharani.

XS
SM
MD
LG