Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 00:36

Idadi ya wapiga kura wanawake imeendelea kuwa juu zaidi kuliko wanaume katika uchaguzi wa rais


Idadi ya wapiga kura wanawake imeendelea kuwa juu zaidi kuliko wanaume katika uchaguzi wa rais
please wait

No media source currently available

0:00 0:04:56 0:00

Idadi ya wapiga kura wanawake imekuwa ni juu zaidi kuliko kwa wanaume katika uchaguzi wa rais Marekani tangu mwaka 1984. Kwa mujibu wa Center for Women in American Politics, wanawake wamekipigia kura chama cha Democratic dhidi ya Republican katika kila uchaguzi wa rais tangu mwaka 1992.

William Frey, Taasisi ya Brookings anaeleza: “Siyo tu wanawake wanajitokeza kwa wingi zaidi kuliko wanaume, lakini wao wanaishi muda mrefu zaidi kuliko wanaume, kwahiyo wale walio katika makundi ya wazee watakuwa na uwakilishi mkubwa zaidi kutoka kwa wanawake.”

William Frey wa taasisi ya Brookings anaelezea takwimu za karibuni za idadi ya watu Marekani na kuonyesha namna kura ya wanawake itakavyokuwa mwaka huu wa 2024. Anasema mwenendo unakipendelea chama cha Democratic, kwa kiasi kwasababu wapiga kura wengi hivi leo ni wanawake ambao wahitimu kutoka katika vyuo.

Forum

Makundi

XS
SM
MD
LG