Katika mfululizo wa makala yetu kuhusu uchaguzi wa Kenya, leo tunaangazia miungano ya kisiasa, baina ya vyama mbalimbali, baadhi vikiwa na itikadi au sera zinazowiana, na vingine vikiungana kwa kila kinachoelezwa kama sababu ya kutafuta uongozi wa kisiasa tu. Tutalenga historia ya miungano hiyo, mafanikio, na changamoto ambazo zimekuwepo kwa miongo kadhaa. Na licha ya bunge la nchi hiyo, kuweka msingi wa kisheria, kuilinda miungano kama hiyo, mapema mwaka huu, wachambuzi wanasema, matatizo bado yameendelea kuwepo. Nampisha mwenzangu BMJ Muriithi asimulie Zaidi.