Bunge la Kenya Jumatano hatimaye limeidhinisha uteuzi wa mawaziri wote 24 kuhudumu kwenye baraza la mawaziri la rais William Ruto.
Hatimaye majaji sita waliokuwa wameteuliwa na tume ya huduma kwa mahakama na majina yao kukataliwa na aliyekuwa rais Uhuru Kenyatta wameapishwa.
Rais mteule wa Kenya William Ruto ametoa mwanga wa agenda ya sera yake ya mambo ya nje katika mahojiano aliyofanya na kituo cha televisheni cha Marekani CNN Jumatano, akiahidi kuongeza mchango wa nchi hiyo katika juhudi za usalama wa kikanda.
Kinara wa Upinzani wa Azimio la Umoja amesema anaheshimu uamuzi wa Mahakama ya Juu lakini ameweka wazi kuwa hakubaliana na uamuzi uliyotolewa.
Uchaguzi Mkuu Kenya: Nini matarajio ya wakazi wa Mombasa, Kenya baada ya kupata gavana mpya? Ungana na Salma Mohamed akikuletea maoni ya wananchi kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa na gavana mpya.
Mahakama ya Juu nchini Kenya siku ya Jumatano imeanza kusikiliza kesi nane zilizounganishwa za kupinga matokeo yaliyomtangaza William Ruto mshindi wa uchaguzi wa urais.
Tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC imekanusha madai kuwa seva zake ziliingiliwa na watu wasiojulikana na kuwezesha utofauti wa matokeo ya uchaguzi kwenye fomu za matokeo zilizopitishwa kwa njia ya elektroniki.
Wakili wa muungano wa Azimio la Umoja Kenya ametetea hatua ya kumshutumu mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi na mipaka, IEBC. wakidai hafai kushikilia wadhifa huo kwa kukiuka katiba.
Uchaguzi katika majimbo ya Mombasa, Kakamega maeneo bunge kadhaa nchini Kenya umefanyika Jumatatu katika hali ya utulivu. Ungana na waandishi wetu wakikusimulia yaliyojiri katika vituo vya kupiga kura.
Kiongozi wa upinzani Raila Odinga, ambaye anapinga kushindwa kwake katika uchaguzi wa urais wa mwezi huu kwenye Mahakama ya Juu, amesema ataheshimu maamuzi ya mahakama – lakini bado anaamini alishinda.
Jopo la Majaji Maarufu wa Afrika limewasili nchini Kenya kufuatilia kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa Urais Kenya 2022, ambapo kongamano linafanyika kabla ya kesi kuanza kusikilizwa Jumanne.
Wananchi watoa tathmini yao juu ya wanasiasa waliohama vyama nchini Kenya mara baada ya uchaguzi. Ungana na mwandishi wa VOA Hubbah Abdi akiwa mitaani kukuletea maoni ya wananchi.
Pandisha zaidi