Upigaji kura ukiendelea siku ya Jumanne katika uchaguzi mkuu wa urais nchini Kenya. Hali ya upigaji kura imeripotiwa kuwa shwari.
Mashindano ya Mabingwa wa Dunia yafanyika Eugene, Oregon Marekani ambako wanariadha kutoka nchi za Afrika wanafanya vizuri.
Msichana kutoka Misri na Mvulana kutoka Marekani ni washindi wa mashindano ya kwanza ya kimataifa kufanyika Marekani.
Zaidi ya waislamu elfu 22 kutoka pembe mbali mbali za Marekani na Canada wamekusanyika kwa siku tatu mjini Baltimore, Maryland kujadili umuhimu wa familia katika uislamu na juhudi za kupambana na chuki.
Barrow mwenye umri wa miaka 56, amepata ushindi wa majimbo ya uchaguzi 36 kati ya 41yaliyotangazwa hadi hivi Jumapili mchana.
Taarifa iliyotolewa na ofisi yake siku ya jumapili inaeleza kwamba “Rais wa Baraza Tawala anakanusha kile shirika la habari la AFP limeripoti kuhusu kushiriki kwa wanajeshi kwenye uchaguzi mkuu ujao.”
Kwa mara ya kwanza baada ya miaka 27 wananchi wa Gambia washiriki kwenye uchaguzi bila ya hofu kutokana na kutokuwepo na jina la kiongozi wa mabavu Yahya Jammeh.
Maafisa wa uchaguzi wana hesabu kura za kila mgombea ambazo ni gololi zilizotumbukizwa kwenye sanduku la kura la kila mgombea na wapigaji kura.
Chama huru cha wafanyakazi wa Afya Sudan wanasema watu watano wameuwawa na polisi kwnye maandamano Jumamosi kupinga mapinduzi ya kijeshi
Kesi iliyokua inasubiriwa kuhusiana na mauwaji ya mwana mapinduzi wa Burkina Faso na Afrika kwa ujumla Thomas Sankara imefunguliwa rasmi mjini Ouagadougu siku ya Jumatatu, bila ya mshukiwa mkuu kutokuwepo, rais wa zamani Blaise Compaore.
Viongozi wa vyama vikuu vya kisiasa nchini Ujerumani wanasema wanaanza mazungumzo ya kujaribu kuunda serikali ya mseto ingawa chama cha SPD kimepata ushindi mdogo kwenye uchaguzi mkuu wa Jumapili.
Rais Joe Biden ahudhuria ibada ya kupokea miili ya wanajeshi wa Marekani walouliwa Kabul, Afghanistan, huku kimbunga kikali cha Ida cha wasili nchi kavu kusini mwa Marekani.
John Mnyika katibu mkuu wa chama cha upinzani cha Chadema anasema viongozi wa chama hicho wanasema wamewasilisha mashtaka mahakamani kupinga tuhuma za ugaidi zilizotajwa dhidi yake.
Viongozi mbalimbali wa nchi za Kiarabu na dunia wanapeleka ujumbe wa pongezi kutokana na ushindi wa Raisi.
Mkuu wa kijeshi wa Kivu kaskazini amewaamrisha wakazi wa Goma mashariki ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kuondoka mara moja.
Israel na kundi la Hamas la Palestina zimetumia silaha nzito nzito wakati ghafla mashambulio yyamegeuka kua mabaya Jumatatu usiku kati ya wahasimu wawili wakuu wa Masharki ya Kati, na kusababisha vifo vya watu 28.
Kwa karibu mwezi mmoja mnamo mwezi huu mtukufu wa Ramadhani Wapalestiina wamekuwa wakipambana wakati wa usiku na polisi wa Israel kwenye uwanja wa al-Aqsa kulalamika dhidi ya hatua kali zilizowekwa na polisi kuingia msikitini humo kutokana na juhudi za kupambana na COVID 19.
Maalim Seif Shariff Hamad kiongozi wa upinzani wa Zanzibar kwa karibu miongo mitatu, afariki akiwa na umri wa miaka 77 baada ya kuugua ugonjwa wa Covid-19.
Maalim Seif alikuwa mmoja kati ya wanasiasa wakongwe na mashuhuri wa Zanzibar na Tanzania aliyegombania mara tano kiti cha urais na kushindwa, lakini kila mara alidai aliibiwa ushindi.
Kaimu waziri mkuu mpya wa Libya Abdul Hamid Dbeibah atoa ahadí ya "kuwa tayari kuwasikiliza na kufanya kazi na wananchi wole wa Libya," alipolihutubia taifa kwa mara ya kwanza Jumamosi usiku, Februari 6, 2021.
Pandisha zaidi