Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 03:42

Rais Barrow aongoza kwenye matokeo ya uchaguzi Gambia


Rais Adama Barrow akizungumza kwenye uwanja wa McCarthy baada ya kupiga kura yake Banjul
Rais Adama Barrow akizungumza kwenye uwanja wa McCarthy baada ya kupiga kura yake Banjul

Rais Adama Barrow wa Gambia anaelekea kupata ushindi mkubwa kwenye uchaguzi wa rais uliofanyika Jumamosi, kufuatana na matokeo ya awali yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi Jumapili.

Barrow mwenye umri wa miaka 56, amepata ushindi wa majimbo ya uchaguzi 40 kati ya 51 yaliyotangazwa Jumapili mchana.

Kiongozi huyo alikabiliwa na upinzani kutoka wagombea watano akiwemo makamu rais wake wa zamani Ousainou Drobe.

Maafisa wa uchaguzi wanasema zoezi la kuhesabu kura limecheleweshwa kutokana na matatizo kadhaa, ikiwa ni pamoja na kukosekana fedha za kutosha kugharamia utaratibu kamili, kujitokeza kwa wapiga kura wengi na mfumo wa kipekee wa upigaji kura nchini humo ambapo watu wanatumia gololi kuwachagua wagombea.

Utaratibu huu wa upigaji kura unatokana na kwamba idadi kubwa ya Wagambia hawajui kusoma na kuandika, ikiwa ni utaratibu ulioanzishwa tangu wakati wa ukoloni wa Uingereza. Hata hivyo maafisa wa uchaguzi wa nchi hiyo wanasema hii itakuwa ni mara ya mwisho kutumia utaratibu huu, kwani unagharimu fedha nyingi na unachukua muda mrefu kuhesabu kura.

XS
SM
MD
LG