Maafisa wa uchaguzi wa Iran wanasema, Raisi alipata asilimia 62 za kura baada ya asilimia 90 za kura kuhesabiwa, na kwamba idadi ya waliojitokeza kupiga kura ilikuwa ndogo.
Shirika la habari la Fars News liliripoti mapema kwamba ni asilimia 37 tu ya wapigaji kura milioni 59 wa taifa hilo walioshiriki kwenye uchaguzi ambao ulishuhudia wagombea kadhaa wakijitoa kabla ya siku ya kupiga kura.
Wachambuzi wanasema uchaguzi huu haujawavutia wa Iran ambao wengi wamekasirishwa na ulaji rushwa, na usimamizi mbaya wa uchumi uliobanwa kutokana na vikwazo vya kiuchumi vya Marekani.
Rais Hassan Rouhani mwenye msimamo wa wastani anaeondoka madarakani baada ya mihula miwili, amewapongeza wananchi kwa kumchagua mtu waliompenda atakaye chukua madaraka mwezi Agosti.
Viongozi mbalimbali wa nchi za Kiarabu na dunia wanapeleka ujumbe wa pongezi kutokana na ushindi wa Raisi.