Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Januari 22, 2025 Local time: 03:43

Wajerumani wasubiri serikali mpya baada ya kutopatikana mshindi kwenye uchaguzi


Olaf Scholz, kati kati, kiongozi wa chama cha SPD mgombea kiti cha Ukansela Ujerumani.
Olaf Scholz, kati kati, kiongozi wa chama cha SPD mgombea kiti cha Ukansela Ujerumani.

Mgombea wa kiti cha ukansela wa Ujerumani na kiongozi wa chama cha Social Democrat, Olaf Scholz, amewahakikishia Wajerumani kwamba ataunda serikali mpya kwa haraka, kabla ya kritsmasi baada ya ushindi mdogo kabisa wa chama chake dhidi ya chama cha Angele Merkel cha CDU.

Kiongozi huyo wa chama cha kati kushoto, SPD alisema hayo baada ya kiongozi wa chama cha CDU Armin Lacshet kukata kutangaza pia kwamba ataunda serikali mpya pia kabla ya krismasi.

Hayo yote yanatokana na kwamba uchaguzi mkuu wa Jumapili haujatoa mshindi wa moja kwa moja na hivi sasa majadiliano yanabidi kufanyika kuundwa serikali ya muungano.

Akizungumza na waandishi habari siku ya Jujamtatu, Bw. Scholz amesema kwamba ushindi mdogo ambao chama chake umepata unampa mamlaka ya kuunda serikali ya mpito, na kwamba wajerumani hawana haja ya kuwa na wasi wasi kwani ni utamaduni wa nchi hiyo kua namazungumzo ya kuundwa serikali baada ya uchaguzi mkuu ulokua na ushindani mkubwa.

Scholz amesema kwamba ana nia ya kuunda serikali kwa haraka iwezekanavyo na vyama vidogo vilivyopata ushindi wa kuweza kuingia bungeni kile cha kutetea mazingira cha Kijani na chama cha Kiliberali cha FDP.

Kiongozi wa chama cha CDU Armin Laschet akiwa pamoja na wakuu wa chama
Kiongozi wa chama cha CDU Armin Laschet akiwa pamoja na wakuu wa chama

Chama cha SPD cha mrengo wa kati kushoto kimepata asili mia 25.7 za kura huku mungano wa wahafidhinaCDU CSU umepata asili mia 24.1. Chama cha kutetea mazingira kimetokea kwa mara ya kwanza nafasi ya tatu kikiwa na asili mia 14.8 za kura na chama cha kiliberali FDP kimepata asili mia 11.5. Chama cha Kijani kinasema kinataka kua na mazungumzo kwanza na chama cha kiliberali cha FDP juu ya suala la serikali ya mungano kabla ya kuzungumza na SPD.

Itakua ni mara ya kwanza baada ya muda mrefu nchini Ujerumani kuhitajika vyama vitatu kuungana ili kuunda serikali. Chama cha kutetea mazingira kimefanya vizuri kwa mara ya kwanza kwa kuchukua nafasi ya tatu iliyokua daima inashikiliwa na FDP.

Mchambuzi wa masuala ya kisiasa mjini Berlin Harrison Mwilima ameiambia Sauti ya Amerika kwamba uwezekano ni mkubwa kwa chama cha SPD kuunda serikali na vyama vya Kijani na FDP kutokana na baadhi ya sera zao zinazofanana.

Anasema ni jambo la kawaida kuwepo na majadiliano kama hayo na Kansela Angela Merkel ataweza kuongeza muda wake madarakani hadi serikali mpya inachaguliwa na hivyo kuvunja rikodi y akua kiongozi aliyetawala kwa muda mrefu Ujerumani.

XS
SM
MD
LG