Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 04:08

CHADEMA inawataka wafuasi kuandamana kupinga kukamatwa kwa Mbowe


Freeman Mbowe kiongozi wa CHADEMA akizungumza na waandishi habari
Freeman Mbowe kiongozi wa CHADEMA akizungumza na waandishi habari

Chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania Chadema kimetoa wito leo Jumamosi kwa wafuasi wake kuandamana kutokana na kukamatwa kwa kiongozi wao Freeman Mbowe.

Viongozi wa chama hicho wanasema wamewasilisha mashtaka mahakamani kupinga tuhuma za ugaidi zilizotajwa dhidi yake.

Mbowe, mwenyekiti wa Chadema alikamatwa siku 10 zilizopita pamoja na maafisa kadhaa waandamanizi wa chama walipokua wanajitayarisha kuhudhuria jopo la hadhara lililopanga kuitisha mabadiliko ya katiba.

Kukamatwa na kusaka nyumba ya kiongozi huyo wakati wa usiku kumezusha wasiwasi miongoni mwa makundi ya kutetea haki na serikali za nchi za magharibi kuhusu utawala wa sheria chini ya uwongozi wa rais mpya Samia Suluhu Hassan.

Wakati wa mkutano na waandishi habari Jumamosi, katibu mkuu wa Chadema, John Mnyika amesema chama chake kimewasilisha mashtaka mahakamani kupinga kesi dhidi ya Mbowe, akisema kumfungulia mashtaka bila ya wakili wake kuwepo ni ukiukaji wa haki zake.

John John Mnyika Katibu mkuu wa chama cha CHADEMA
John John Mnyika Katibu mkuu wa chama cha CHADEMA

Mnyika aliwahimiza pia wafuasi wa chama na waungaji mkono kuanda maandamani ya amani kulalamika dhidi ya mashtaka yaliyotungwa wakati kesi ya Mbowe itakaposikilizwa mahakamani Augusti 5.

Mbowe mwenye umri wa miaka 59 alifunguliwa mashtaka Jumatatu kuhusu ugaidi, utakasaji fedha na njamana ya kutaka kufanya mauwajisiku ya jumatatu, mashtaka ambayo haimruhusu mtu kuachiwa kwa dhamana nchini Tanzania.

Wakosowaji wamesema hatua dhidi ya kiongozi huyo wa uopinzani ni kurudisha tena mfumo wa ukandamizaji w arais wa zamani wa Tanzania marhemu John Pombe Magufuli na kuonesha kwamba ni machache tu yaliyobadilika chini ya Bi. Hassan.

Marekani imeeleza wasiwasi wake kutokana na kukamatwa kwa Mbowe na kumhimiza rais Hassan aliyechukua madaraka mwezi March kuhakikisha kuna uhuru kwa watanzania wote.

XS
SM
MD
LG