Sehemu nyingine ya mkataba huo, ni tamko la kikatiba, linalotarajiwa kusainiwa mapema Ijumaa.
Matokeo hayo ni hatua ya kusonga mbele katika siasa za mpito nchini Sudan ambapo kulikuwa na miezi kadhaa ya machafuko tangu jeshi kumpindua kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir.
Mkataba wa kushirikiana katika madaraka ni pamoja na kuundwa kwa baraza la kujitegemea la pamoja lililopewa jukumu la kuongoza nchi hiyo kwa miaka isiyopungua mitatu kabla ya uchaguzi mpya kufanyika.
Pande zote mbili pia zimekubaliana kuwepo uchunguzi huru juu ya vitendo vya jeshi kuwashambulia waandamanaji Juni 2019, ambapo waandaaji wa maandamano wanasema watu 128 walikufa huku wizara ya afya ikisema idadi ya waliokufa ilikuwa watu 61.