Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumapili, Novemba 24, 2024 Local time: 00:47

Aboul Gheit amekutana na baraza la jeshi linalotawala Sudan


Ahmed Aboul Gheit, katibu mkuu wa umoja wa nchi za falme za kiarabu
Ahmed Aboul Gheit, katibu mkuu wa umoja wa nchi za falme za kiarabu

Kiongozi huyo wa cheo cha juu katika nchi za falme za kiarabu aliwaambia waandishi wa habari alisikiliza mtazamo wa Jenerali Abdel Fattah Burhan kuhusu matatizo ya Sudan na yeye alimweleza mtazamo wa umoja wa falme za kiarabu kuhusiana na hali hii ya kisiasa nchini Sudan

Katibu mkuu wa umoja wa nchi za falme za kiarabu alifanya mazungumzo mjini Khartoum Jumapili na baraza la jeshi linalotawala Sudan. Ahmed Aboul Gheit aliwaambia waandishi wa habari kwamba mkutano wake na Jenerali Abdel-Fattah Burhan ulikuwa na matumaini na kwamba walibadilishana mawazo juu ya namna ya kupata auheni katika matatizo ya kisiasa ya Sudan.

Aboul Gheit alieleza kuwa alisikiliza mapendekezo na mtazamo wa Jenerali Abdel Fattah Burhan kuhusu hali nchini Sudan na yeye alimweleza wazi mtazamo wa umoja wa falme za kiarabu akivilenga vikosi vya usalama Sudan vilikiuka kutawanya kambi ya waandamanaji mjini Khartoum hapo Juni 3 mahala ambako waandamanaji walikuwa wakifanya maandamano yao ya kukaa chini wakitoa wito kwa baraza la jeshi kukabidhi madaraka kwa utawala wa kiraia.

Zaidi ya watu 100 wameuwawa na mamia walijeruhiwa tangu wakati huo kulingana na waandaaji wa maandamano hayo. Maafisa wa Sudan wanaeleza ni watu 61 pekee ndio walifariki wakiwemo watatu kutoka vikosi vya usalama.

XS
SM
MD
LG