Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 18:46

Jeshi, upinzani Sudan vyaunda kamati kuchunguza mashambulizi dhidi ya waandamanaji


Waandamanaji nchini Sudan wakiwa wamejipanga mbele ya makao makuu ya jeshi, Khartoum, Sudan, Mei, 2019.
Waandamanaji nchini Sudan wakiwa wamejipanga mbele ya makao makuu ya jeshi, Khartoum, Sudan, Mei, 2019.

Kamati ya kijeshi inayosimamia serikali ya mpito nchini Sudan, imeunda kamati ya pamoja na muungano wa upinzani unaopigania uhuru na mabadiliko, kuchunguza mashambulizi yanayowalenga waandamanaji.

Mwanachama wa kamati hiyo ya jeshi amewaambia waandishi wa habari kwamba kamati hiyo imepewa jukumu la kuhakikisha kwamba hakuna jaribio lolote la kuwatawanya waandamanaji.

Waandamanaji hao bado wamepiga kambi nje ya wizara ya ulinzi mjini Khartoum tangu April 6.

Milio ya risasi ilisikika mjini Khartoum, Jumatatu usiku baada ya kikosi cha jeshi cha masuala ya dharura, kinachoongozwa na naibu kiongozi wa baraza la kijeshi.

Kikosi hicho kinafanya doria mjini humo na kurusha mabomu ya kutoa machozi, kwa lengo la kuwatanya waandamanaji.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.

XS
SM
MD
LG