Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 19:14

Wananchi Sudan waendelea kushinikiza jeshi kukabidhi madaraka kwa raia


Waandamanaji nchini Sudan wakipaza sauti mbelel ya vikosi vya ulinzi wakati maandamano yakiendelea Khartoum, Sudan, Aprili. 15, 2019.
Waandamanaji nchini Sudan wakipaza sauti mbelel ya vikosi vya ulinzi wakati maandamano yakiendelea Khartoum, Sudan, Aprili. 15, 2019.

Waandamanaji nchini Sudan wamechukua hatua kuwazuia wanajeshi kuwaondoa kwa nguvu waandamanaji wenzao waliopiga kambi nje ya Wizara wa Ulinzi.

Walioshuhudia harakati hizo wanasema wanajeshi walikuwa wanajipanga kuingia katika eneo hilo kutoka sehemu tatu tofauti hii leo huku trekta zikiondosha mawe na vizingiti vilivyowekwa.

Waandamanaji walishikana mikono na kufanya mduara kulizunguka eneo waliokuwa wamekaa waandamanaji ili kuwazuia wanajeshi kuingia.

Wananchi hao wamekuwa wakihimiza kuwepo mageuzi ya mara moja ya utawala wa kiraia baada ya kupinduliwa Rais Omar al-Bashir wiki ilyiopita.

Mamia ya waandamanaji walionekana wakielekea katika makao makuu ya Jeshi ili kuwaunga mkono wenzao na kuitikia wito wa Chama cha wataalam, SPA.

Wakati hayo yakiendelea wanaharakati na serikali za nchi za Magharibi zinaendelea kuwahimiza wanajeshi kukabidhi madaraka kwa serikali mpya ya kiraia mara moja.

Chama cha SPA kinalihimiza baraza la kijeshi lililokutana na wawakilishi wao na vyama vya kisiasa hapo Jumapili kukabidhi mara moja utawala kwa raia.

Uingereza Marekani na Norway zimelihimiza pia baraza hilo la kijeshi na vyama vya kisiasa kuanza mazungumzo juu ya kipindi cha mpito cha nchi hiyo kuelekea utawala wa kiraia.

Imetayarishwa na mwandishi wetu, Abdushakur Aboud, Washington, DC

XS
SM
MD
LG