Maandamano hayo yalianza Disemba 19, 2019, kutokana na kupinga ongezeko la bei ya mikate na mafuta ya petroli na tangu hapo kuendelea hadi Jumatano wakishinikiza rais huyo ajiuzulu baada ya miaka 30 madarakani.
Waandamanji wamekuwa wakiitikia wito wa chama cha wanataaluma wa Sudan kufanya maandamano na kukaa nje ya makao makuu ya jeshi la nchi hiyo.
Naye mwandishi wa Sauti ya Amerika mjini Khartoum, Dama Moheideen anasema inaonekana hakuna kiongozi wa kweli wa vuguvugu hilo.
Walioshuhudia maandamano hayo wamesema majaribio ya baadhi ya askari kuwaondoa waandamanji hao yaliwasababisha wanajeshi kuwalinda hao waandamanaji.
Imetayarishwa na Mwandishi wetu, Washington, DC.