Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Desemba 26, 2024 Local time: 06:36

Rais wa Sudan anawakemea waandamanaji wanaomtaka ajiuzulu


Rais wa Sudan, Omar al-Bashir
Rais wa Sudan, Omar al-Bashir

Akiwahutubia wanajeshi kwenye kambi ya kijeshi karibu na mji wa Atbara alisema “hatuna tatizo kwa sababu jeshi halichukua hatua kuwasaidia wasaliti lakini linafanya kazi kulilinda taifa na ustawi wake"

Rais wa Sudan Omar al-Bashir anaekabiliwa na upinzani mkali wa maandamano kuwahi kutokea tangu alipochukua madaraka mwaka 1989 alikaidi wito unaomtaka ajiuzulu. Wakati huo huo vikosi vya usalama vinaendelea kupambana na waandamanaji ambapo Jumanne viliwafyatulia mabomu ya kutoa machozi waandamanaji katika mji wa mashariki wa al-Qadarif.

Akiwahutubia wanajeshi kwenye kambi ya kijeshi karibu na mji wa Atbara ulioko kaskazini-mashariki ya mji mkuu Khartoum Rais Bashir alikemea wito wa waandamanaji unaomtaka ajiuzulu na kukabidhi madaraka kwa jeshi.

Rais wa Sudan, Omar Hassan al-Bashir
Rais wa Sudan, Omar Hassan al-Bashir

Kufuatana na sehemu ya hotuba yake iliyotangazwa na TV yenye uhusiano na chama tawala Rais Bashir alisema “hatuna tatizo kwa sababu jeshi halichukua hatua kuwasaidia wasaliti lakini linafanya kazi kulilinda taifa na ustawi wake.

Bashir, Jenerali wa zamani wa jeshi aliingia madarakani kwa njia ya mapinduzi yaliyoungwa mkono na kundi la ki-Islam na amefanya uchaguzi kadhaa uliompatia ushindi ambapo wapinzani wake wanasema haukuwa huru na wenye usawa.

Mashahidi walisema wanajeshi na maafisa wa usalama wamefunga njia muhiumu na kutawanya maandamano wakitumia risasi za moto pamoja na gesi ya kutoa machozi na maguruneti.

Waandamanaji wanaoipinga serikali ya Sudan
Waandamanaji wanaoipinga serikali ya Sudan

Maandamano yaliyofanyika Jumanne huko al-Qadarif ndiyo yalikuwa makubwa zaidi kufanyika katika wiki za karibuni.

Video iliyosambazwa kwenye mtandao wa kijamii ilionesha mamia ya watu wakitamka maneno “uhuru, amani, sheria na mapinduzi ni chaguo la wananchi". Shirika la habari la Reuters halikuweza kupata uthibitisho huru kuhusu wa picha hizo.

XS
SM
MD
LG