Upatikanaji viungo

Breaking News
Alhamisi, Januari 23, 2025 Local time: 20:25

Rais wa Sudan anasema wapinzani wanatumiwa na watu wa nje


Rais wa Sudan, Omar Hassan al-Bashir
Rais wa Sudan, Omar Hassan al-Bashir

Rais Bashir aliwaeleza wafuasi wake katika mji wa Wad al-Madani kwamba hali ya kuporomoka kwa uchumi ilikuwa ni matokeo ya vizuizi vya kiuchumi kutoka nje ya Sudan

Rais wa Sudan Omar Hassan al-Bashir aliuambia umati wa wafuasi wake kwamba jitihada zao za kujitokeza kumsikiliza ni majibu yenye nguvu kwa wasaliti wote, waharibifu wa makusudi na mamluki ambao wamekuwa wakiandamana dhidi ya serikali yake.

Kanda ya video iliyobandikwa kwenye mtandao wa kijamii ilionyesha umati mkubwa wa waandamanaji katika mji mkuu Khartoum siku ya Jumanne wakiandamana dhidi ya hali ya kiuchumi na kumtaka rais aachie madaraka.

Kundi la vyama vya kisiasa na vyama vya wafanyakazi viliwasihi wafuasi wao kujitokeza mitaani na kumtaka Bashir ajiuzulu.

Omar al-Bashir
Omar al-Bashir

Wakati huo huo Rais Bashir alihutubia umati wa wafuasi wake katika mji wa Wad al-Madani katika jimbo la Jezira akiwaeleza kwamba hali ya kuporomoka kwa uchumi ilikuwa ni matokeo ya vizuizi vya kiuchumi kutoka nje ya Sudan.

Marekani iliondoa vikwazo vya kiuchumi dhidi ya Sudan mwezi Oktoba lakini sarafu ya Sudan imepoteza thamani yake kwa kiwango kikubwa.

Bashir pia aliwakemea wapinzani wake, akisema wanatumiwa na watu wa nje. “Anasema kwamba wafuasi wake watasalimu amri kwa mwenyenzi mungu pekee na anawashukuru kwa jitihada yao kujitokeza kumkaribisha na kumuunga mkono dhidi ya kile anachokiita wasaliti, mawakala, waharibifu wa makusudi na mamluki wa watu wa nje”.

Vyombo vya habari vya kiarabu viliripoti kwamba vikosi vya usalama vya Sudan vinavyomtii Bashir viliwekwa tena kwenye maeneo ya mpakani na maeneo mengine yenye matatizo nchini humo kuzima maandamano mjini Khartoum.

Rais Bashir ambaye anatafutwa na mahakama ya kimataifa ya uhalifu kwa ukiukaji wa haki za binadamu katika jimbo la Darfur nchini Sudan, ameiongoza Sudan tangu mapinduzi ya mwaka 1989. Wabunge hivi karibuni walifanya marekebisho ya katiba ili kumruhusu Bashir kuwania tena uongozi mwaka 2020.

XS
SM
MD
LG