Serikali ya Sudan inaongeza juhudi za kukabiliana na ghasia kwa kutumia nguvu na kumaliza maandamano yaliyoenea nchini humo kwa mujibu wa muandamanaji Nour El Din aliyehojiwa na kipindi cha VOA.
El Din alikieleza kipindi cha South Sudan in Focus cha VOA siku ya Jumatatu kwamba polisi wanawasaka waandamanaji na wanatumia bunduki zao hata ndani ya nyumba. Aliomba jina lake kamili lisitumiwe kwenye taarifa hii. El Din mhandisi wa madini ambaye alishiriki maandamano katika mji mkuu wa Sudan wikiendi iliyopita alieleza maandamano yaliandaliwa na muungano wa wasomi wa Sudan-SDA na muungano wa vyama huru vya wasomi nchini humo.
Alisema maandamano yalifanyika huko Bory na chuo kikuu cha Khartoum mahala ambako waalimu na watawala wa chuo kikuu walijumuika kwenye maandamano. El Din alieleza serikali ilitumia nguvu kupita kiasi pamoja na gesi ya kutoa machozi dhidi ya waandamanaji.
Maandamano yalianza disemba 19 mwaka 2018 baada ya serikali kupandisha bei ya mkate. Zaidi ya watu 800 wamekamatwa kote nchini kwa kusihiriki kwenye maandamano.