Sameh Shoukry, ambaye pia ni mkuu wa ujasusi wa Misri, ameahidi kuisaidia Sudan, kutatua mgogoro wa ndani, katika kikao na Rais wa Sudan Omar Al-Bashir, mjini Khartoum.
Sudan inakabiliwa na wimbi la maandamano ya raia yenye lengo ya kuuangusha utawala wa Rais Omar Al-Bashir, kufuatia kupanda kwa bei ya mkate, uhaba wa chakula na mafuta.
Vyanzo vya habari nchini Sudan vinasema kwamba hali ya maandamano nchini Sudan inaweza kutatiza utulivu nchini Misri.
Vyombo vya usalama nchini Sudan vimesema kuwa watu 19 wameuwawa tangu machafuko hayo yaanze Disemba, wakati shirika la kutetea haki za binadamu imetoa idadi ya watu 37, ikinukuu ripoti za kuaminika.
Rais Bashir ametaja wanao andamana kuwa wasaliti na mamluki wanaotumiwa na watu wanaotaka kuangusha utawala wake.
Wakati huohuo Rais Bashir ameahidi kufanya mabadiliko makubwa ya kiuchumi.