Siku tano baada ya wanajeshi waliofanya mapinduzi kumuondoa Bashir , 75, madarakani na kumweka kizuizini nyumbani kwake.
Shirika la habari la Reuters imeripoti kuwa familia yake nchini Sudan, Jumatano, imethibitisha kuwa Bashir alikuwa akishikiliwa chini ya ulinzi mkali katika kasri ya rais.
Wakati huohuo vyombo vya habari vimeripoti kuwa waandamanaji bado Jumatano wanaendelea kupiga kambi nje ya makao makuu ya jeshi.
Waandamanaji hao wanashinikiza kuundwa kwa serikali ya kiraia na kulitaka jeshi kukabidhi madaraka kwa amani.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.