Upatikanaji viungo

Breaking News
Jumatano, Desemba 25, 2024 Local time: 18:50

Mvutano wa kisiasa Sudan bado ni kitendawili


Waandamanaji na wanaharakati nchini Sudan bado hawaridhishwe na mfumo wa baraza la mpito
Waandamanaji na wanaharakati nchini Sudan bado hawaridhishwe na mfumo wa baraza la mpito

Muungano wa wanaharakati na makundi ya upinzani ulituma mswada wa nakala ya katiba kwa baraza la jeshi siku ya Alhamis ulioeleza majukumu ya baraza la mpito litakalokuwa na madaraka kamili wakati wa kipindi cha mpito

Baraza la muda la kijeshi nchini Sudan TMC siku ya Jumapili lilieleza kwamba litachapisha maoni yake juu ya muelekeo wa kipindi cha mpito cha nchi hiyo siku ya Jumatatu katika hatua yake mpya katika mashauriano na vyama vya upinzani baada ya kuondolewa madarakani rais wa muda mrefu nchini humo Omar al Bashir.

Kulingana na shirika la habari la Reuters waandamanaji na wanaharakati wamekuwa wakishauriana na TMC kuunda baraza la pamoja litakalowashirikisha raia na jeshi kuongoza hadi uchaguzi utakapofanyika nchini humo. Lakini vyama vinakwama kusonga mbele juu ya nani atakayedhibiti baraza jipya na kuhusu hali ya baadae ya serikali ya mpito.

Muungano wa wanaharakati na makundi ya upinzani-DFCF ulituma mswada wa nakala ya katiba kwa baraza la jeshi siku ya Alhamis ulioeleza majukumu ya baraza la mpito litakalokuwa na madaraka kamili wakati wa kipindi cha mpito. DFCF ilitarajia majibu ili mashauriano yasonge mbele.

Mswada huo hauelezi nani ataliongoza baraza la mpito lakini unaelezea majukumu ya baraza la mawaziri na wabunge wake 120. Luteni Jenerali Shams El Din Kabbashi, msemaji kwa baraza la kijeshi alieleza kwamba nakala ilikuwa nzuri akiongeza kwamba baraza lilikubaliana juu ya vipengele vyake kadhaa na pia lilikuwa na mapendekezo yake kwenye baadhi ya vipengele.

XS
SM
MD
LG