Hatua hiyo inafuatia wito wa viongozi wa upinzani kwa waandamanaji washiriki maandamano mengine makubwa kuwashinikiza majenerali wa jeshi kuharakisha mchakato wa kukabidhi madaraka kwa serikali ya kiraia.
Huku wakiimba nyimbo za kuunga mkono serikali ya kiraia na wakipepea bendera za Sudan, waandamanaji hao ambao wengi wao ni vijana waliungana na wenzao kwa kukaa nje ya makao makuu ya jeshi hilo wakati giza lilipoingia.
Eneo hilo ndio limekuwa sehemu kuu ya vuguvugu la maandamano yaliomtoa madarakani kiongozi wa muda mrefu Omar al -Bashir, mwezi Aprili 2019, na kutaka majenerali wa jeshi waliochukua nafasi yake kukabidhi madaraka kwa raia.
Imetayarishwa na mwandishi wetu, Washington, DC.